Na Nyeneu, P. R
Katika miaka mitano iliyopita tafiti mbalimbali za Magonjwa ya Kinywa na Meno Mkoa wa Manyara zimeonyesha kuongezeka kwa asilimia Hamsini na Moja (51%) Walieleza madaktari Catherine Mganga kutoka kitengo cha Meno Hospitali ya wilaya ya Babati na Daktari Mahendeka Mratibu wa afya ya kinywa na Meno kutoka ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Manyara. Katika tafiti hizo, takwimu pia zinaonesha magonjwa yanayoongoza ni kutoboka kwa meno, Magonjwa ya Ufizi, na mengine ni mpangilio mbaya wa Meno, kuzidi kwa Madini ya floraidi (Floride) kwenye meno ambayo husababisha au hubadili rangi ya meno pia ni pamoja na ajali zinazohusisha maeneo ya kinywa na meno.
Meno yaliyoharibika kwa kubadilika rangi baada ya kuzidi madini ya Floride
Kwa kawaida matibabu ya magonjwa hayo hupatikana katika vituo vya kutolea huduma za kinywa na meno ambazo ni Hospitali zote za Halmashauri za Mkoa wa Manyara, Vituo vya Afya vya Magugu na Katesh na Kliniki za Kinywa na Meno za Eagle Polyclinic na Oasis Dental Clinic. Alisema Dkt. Mahendeka. Matibabu hayo ni pamoja na Kung'oa jino, Kuziba jino, kusafisha na kutoa ushauri wa Kinywa na Meno wa Jamii nzima.
Ung'oaji wa Jino kwa Mama Mjamzito ni salama kabisa na ni Muhimu iwapo Mjamzito anasumbuliwa na Jino (Meno)
Aidha Wataalamu hao waliongeza kuwa kumekuwa na nadharia potofu hususani matibabu ya meno hasa hasa kung'oa. Imani hizo zinatokana na mazoea mbalimbali katika jamii. Kitaalamu meno yoyote yanaweza kung'olewa wakati wowote. Baadhi ya Imani hizo potofu ni: -
na zingine nyingi.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati