• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Biashara
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara

MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII- TASAF

  • Utangulizi 

Halmashauri ya Mji wa Babati ni miongoni mwa Halmashauri/Manispaa na Miji 27 zilizoko katika awamu ya tatu ya utekelezaji.

Utekelezaji wa mpango wa TASAF awamu ya tatu ndani ya Halmashauri ya Mji wa Babati ulianza rasmi tarehe 15 Julai, 2014 kwa kuzitambua na kuandikisha kaya maskini katika vijiji 6 na Mitaa 15 kati ya vijiji 13 na Mitaa 35 iliyopo katika Halmashauri. Kwa sasa mpango umefika kwenye vijiji vyote 13 na mitaa 35 ya Halmashauri ya Mji wa Babati. Mpango huu umewafikia walengwa 2319.

  • Madhumuni ya Mpango
  • Madhumuni ya Mpango huu ni kuziwezesha kaya maskini kupata mahitaji ya msingi na fursa za kujiongezea kipato na kuweka akiba. Walengwa wa mpango huu ni kaya maskini katika jamii kwa maeneo ya utekelezaji yaliyoainishwa.
  • Walengwa wa Mpango

Walengwa wa Mpango wanatoka Mitaa 35 na Vijiji 13 vifuatavyo:-  Babati Mjini, Hangoni, Kwere, Maisaka B, Majengo, Mrara, Waang'waray, Bagara ziwani, Komoto, Miomboni, Mjimpya, Nakwa, Negamsi, Ngarenaro, Nyanguu, Oysterbay, Ayabadinay, Bonga mjini, Dawar, Haraa, Himiti, Kandaka, Waang’boo, Kiongozi, Maisaka A, Maisaka kati, Malangi, Mruki, Sawe, Chemchem, Mutuka, Arri, Balowa, Halla, Maweni, Mkuyuni A, Mkuyuni B, Nangara Kati, Ziwani, Daghailoy, Imbilili, Sigino, Singu, Gendi Barazani, Gendi Kuu , Majengo Mapya, Managhat na Nyawari.

  • Uhawilishaji wa fedha.

Katika uhawilishaji wa fedha, Halmashauri ya Mji wa Babati inahawilisha fedha kwa njia 2 ambazo ni kwa njia ya Fedha taslim na njia ya kielektroniki ambapo jumla ya walengwa 818 wanapokea fedha zao kwa njia fedha taslim na 1,501 kwa njia ya kielektroniki.

Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024, Halmashauri ya Mji wa Babati ilipokea kiasi cha Tsh. 686,373,242/= kwa ajili ya zoezi la uhawilishaji fedha kwa walengwa.

  • Utekelezaji wa miradi ya kutoa ajira za muda

Miradi hii inatekelezwa na kaya zilizoandikishwa kwenye mpango zenye watu  wenye uwezo wa kufanya kazi kwa kutumia teknolojia ya nguvu kazi.

Miradi hii inatekelezwa kwa kufuata kanuni na taratibu za utekelezaji wa miradi ya ajira za muda kwa washiriki kama zilivyoainishwa kwenye miongozo ya utekelezaji.

Madhumuni ya miradi ya kutoa ajira za muda ni kutoa fursa zifuatazo:

  • Kutoa ajira ya muda kwa walengwa ili kuongeza kipato na matumizi kwenye Kaya,
  •  Kupata  miundombinu katika  jamii, na
  • Kuongeza ujuzi kwa walengwa.

Halmashauri ya Mji wa Babati ilianza kutekeleza Miradi ya kutoa ajira za muda kwa mwaka 2022/2023 ambapo jumla ya miradi 31 iliibuliwa na kutekelezwa miradi 29. Katika utekelezaji wa miradi hii, jumla ya Tsh. 258,372,000 zilizipwa kama ujira kwa kaya 1,647 zilizoshiriki katika kazi za kutoa ajira za muda. Kwa mwaka 2023/2024, jumla ya miradi 33 iliibuliwa ambapo kati ya hiyo kuna miradi 7 ambayo imeanza kutekelezwa.

  • Uanzishwaji wa vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana.

Mpango wa Kuhamasisha Jamii Kuweka Akiba na Kuwekeza  ni mojawapo ya mbinu za kujenga uwezo iliyobuniwa ili kujenga tabia na utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza kwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Mijini na Vijijini.

Mpango huu utabadilisha mbinu za zamani za kuweka akiba na kuwekeza kuwa mbinu za kisasa amabapo akiba hiyo inaweza baadae kuwekezwa kupitia taasisi za fedha ili kukuza kipato cha kaya na kuondokana na umaskini.

Mkazo unawekwa katika kuhamasisha uwekaji wa akiba na kujenga uwezo kupitia mafunzo mbalimbali yatakayotolewa kwa Vikundi vya walengwa vitakavyoundwa.

Halmashauri ya Mji wa Babati katika kutekeleza program hii, imeanzisha vikundi vya walengwa 43 vyenye jumla ya walengwa 555. Vikundi hivi vimejengewa uwezo kwa kupewa mafunzo na kuwezesha vitabu vya kuweka kumbukumbu za kifedha. Aidha TASAF itagharimia utengenezaji wa kasiki kwa ajili ya kutunzia fedha ambapo baadaye itawawezesha kufungua akaunti katika taasisi za kifedha.

  • Mafanikio

Pamoja na changamoto mbalimbali zinazojitokeza, yapo mafanikio makubwa miongoni mwa walengwa na jamii kwa ujumla kama ifuatavyo;

  • Ongezeko la wanafunzi na watoto wa chini ya miaka 5 wanaohudumiwa na TASAF ambapo wanafunzi wameongezeka kutoka 951 hadi 2,660 wanapokea ruzuku ya masharti na watoto kutoka 171 hadi 450 wanapokea ruzuku ya masharti.
  • Ongezeko la kaya zinazojiunga na Mfuko wa Afya ulioboreshwa kutoka 130 hadi 357.
  • Asilimia 87 ya walengwa kuweza kumudu gharama mbalimbali za maisha
  • Kuwekeza katika shughuli za kiuchumi, kama vile kilimo, mifugo midogomidogo na biashara ndogondogo.
  • Kuboresha makazi kwa kujenga nyumba bora.
  • Kuongezeka kwa ujuzi kupitia ajira za muda ambapo jumla ya kaya 1,647 zimenufaika.

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili 2025. May 08, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR CONSTRUCTION SUPERVISION CONSUTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BABATI TOWN UNDER TACTIC PRJECT TIER 2 March 07, 2025
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI 2025. May 13, 2025
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI 2025. May 13, 2025
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Kikao kazi cha maazimio ya mikakati ya kupunguza Ukatili wa kijinsia.

    May 29, 2025
  • Wakazi wa Halmashauri ya Mji Babati wanufaika na Gulio la Gendi.

    May 28, 2025
  • Elimu ya Matumizi sahihi ya Dawa za Binadamu imetolewa kwa Watumishi wa Halmashauri ya Mji Babati.

    May 28, 2025
  • Baraza maalum la Hoja Halmashauri ya Mji wa Babati.

    May 27, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Babati 2024
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati