• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Biashara
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Elimu Sekondari



MUUNDO WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI
UTANGULIZI
Halmashauri ya Mji wa Babati ina jumla ya Shule za Sekondari 18 kati ya hizo Shule 12 ni za Serikali na Shule 06 ni za Binafsi. Shule za serikali zina jumla ya Wanafunzi 6177 kati yao wavulana 2655 na wasichana 3522 na shule za Binafsi zina Jumla ya 2231 kati yao wavulana ni 1132 na wasichana ni 1100. Halmashauri ina jumla ya walimu 375 katika shule za sekondari za serikali.
 
MAJUKUMU YA MKUU WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI WA HALMASHAURI
Ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Halmashauri. Majukumu yake ni pamoja na:-
  • Kuiwakilisha Wizara katika halmashauri kuhusu masuala ya elimu sekondari .
  • Kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni zinazoongoza utoaji wa elimu ya sekondari
  • Kusimamia upanuzi wa elimu ya sekondari katika halmashauri
  • Kusimamia haki na maslahi ya walimu na watumishi wengine wa ngazi ya elimu ya sekondari katika halmashauri
  • Kusimamia na kudhibiti akaunti ya elimu ya sekondari na kuhakikisha kuwa fedha za elimu ya sekondari zinatumika kama ilivyokusudiwa
  • Kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya sekondari
  • Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya elimu ya sekondari katika halmashauri
  • Khakikisha kuwa shule zote za sekondari katika halmashauri zinainua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kujifundishia ikiwa ni pamoja na utunzaji wa madarasa, nyumba za walimu, maabara, maktaba na vyoo
  • Kusimamia tathmini  ya wazi ya utendaji kazi (Open Performance Review and Appraisal System -OPRAS)  kwa walimu na watumishi wa sekondari
  • Kuhimiza udhibiti wa nidhamu ya walimu, watumishi na wanafunzi wa shule  za sekondari katika halmashauri
  • Kumshauri mkurugenzi wa halmashauri kuhusu masuala yote ya elimu ya sekondari 
  • Kufanya kazi nyingine kama itakavyoelekezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri

MAJUKUMU YA AFISA ELIMU TAALUMA SEKONDARI WA HALMASHAURI
Afisa Elimu Taaluma wa Sekondari anatekeleza majukumu yafuatayo katika Halmashauri:-
  • Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule za sekondari.
  •  Kubuni mipango ya mitihani ya elimu ya sekondari na kusimamia utekelezaji wake

  • Kuhakikisha kuwa walimu na watumishi wengine wa shuke za sekondari wanafanyiwa tathmini ya wazi ya utendaji kazi (Open Performance Review and Appraisal System-OPRAS)

  • Kubuni na kuratibu mipango ya mafunzo kazini kwa walimu na watumishi wengine wa shule za sekondari.

  • Kuratibu mashindano ya michezo na Taaluma ya shule za sekondari katika Halmashauri (UMISSETA).

  • Kuratibu utoaji wa huduma mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za sekondari katika Halmashauri

  • Kufanya kazi nyingine atakazopewa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Afisa Elimu wa Elimu ya Sekondari wa Halmashauri.


MAJUKUMU YA AFISA ELIMU VIFAA NA TAKWIMU WA SEKONDARI WA HALMASHAURI
Majukumu ya Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Sekondari wa Halmashauri ni haya yafuatayo:-
  • Kuratibu, kukusanya na kuchambua takwimu za elimu ya Sekondari katika Halmashauri.
  • Kusimamia na kufuatilia ukarabati, upanuzi na ujenzi wa shule za sekondari.
  • Kufanya makisio ya mahitaji ya walimu kimadaraja na kimasomo.
  • Kuagiza na kusambaza vifaa vya shule kulingana na mahitaji ya Halmashauri na shule.
  • Kufuatilia mapato na matumizi ya fedha katika shule za sekondari.
  • Kufuatilia utekelezaji wa huduma mbalimbali kwa wanafunzi
  • Kufanya kazi nyingine kama itakavyoelekezwa na Afisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri au Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. 

MAJUKUMU YA AFISA ELIMU KATA
Majukumu ya Afisa Elimu Kata yamegawanyika katika majukumu ya kiutawala na majukumu ya kitaaluma kama inavyofafanuliwa hapa chini:-

a) Majukumu ya Kiutawala
  • Kusimamia utekelezaji wa sera, kanuni na miongozo ya usimamizi na uendeshaji wa elimu katika kata.
  • Kuwa mshauri wa Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) katika mambo yanayohusu 
  • Elimu ya Sekondari katika Kata.
  • Kushirikiana na Kamati ya maendeleo ya Kata na Afisa Elimu wa Sekondari kuchagua 
  • maeneo yanayopendekezwa kujenga shule mpya na kuendeleza ujenzi wake.
  • Kufanya ufuatiliaji wa shughuli za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule.
  • Kuhamasisha jamii kuchangia fedha na nguvukazi katika ujenzi wa shule mpya na kuimarisha miundombinu ya shule zilizopo.
  • Kupokea na kupitisha Mpango Shirikishi wa maendeleo ya shule, bajeti na taarifa za utekelezaji
  • Kushirikiana na uongozi wa Kata na vijiji kuhakikisha wanafunzi wanaojiunga na Kidato cha kwanza, wanaandikishwa, wanahudhuria na kumaliza elimu ya sekondari bila vikwazo vyovyote.
  • Kuratibu upatikanaji wa takwimu za shule za sekondari kwa kushirikiana na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Sekondari wa Halmashauri.
b) Majukumu ya Kitaaluma
  • Majukumu ya kitaaluma ya Afisa Elimu Kata ni pamoja na:-
  • Kushirikiana na uongozi wa shule za sekondari katika kupanga na kusimamia mbinu mpya za kusimamia taaluma shuleni.
  • Kushirikiana na menejimenti za Shule za Sekondari katika kuweka mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
  • Afisa Elimu Kata ni mkaguzi wa ndani. Hutoa ushauri wa utoaji wa taaluma katika shule za sekondari na kuwasilisha taarifa kwa Afisa 
  • Elimu Sekondari wa Halmashauri. Katika utekelezaji wa jukumu hili atawasiliana na Mkuu wa Shule kupata kumbukumbu zote muhimu.
MAJUKUMU YA BODI YA SHULE
Kila shule ya Sekondari katika Halmashauri inapaswa kuwa na Bodi ya shule. Bodi za shule zimeanzishwa kwa mujibu wa kifungu
 cha 39 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kikisomwa pamoja na kanuni za elimu. Pamoja na mambo mengine. Bodi ya Shule itakuwa na majukumu ya kupitia na kuelekeza Wakuu wa Shule kuhusu masuala ya fedha za shule.

Katika kutekeleza majukumu yake, bodi inatakiwa:-
  • Kupitia, kujadili na kuidhinisha bajeti ya shule
  • Kupitia na kujadili ripoti za fedha za robo mwaka na za mwisho wa mwaka.
  • Kuteua kamati ndogo ya kusimamia mfuko wa maduhuli, manunuzi na  ujenzi
  • Kujadili na kupitisha maombi ya manunuzi ya bidhaa, huduma, ujenzi, vifaa na vifaa kufundishia na kujifunzia.
 MAJUKUMU YA MKUU WA SHULE
  • Kusimamia utekelezaji wa mtaala
  • Kuwa Mkaguzi wa ndani na wa awali wa ufundishaji wa walimu.
  • Kupokea na kusajili wanafunzi wapya.
  • Kusimamia mali zote za shule.
  • Kutafsiri,kusimamia na kutekeleza Sera, sharia, ya Elimu, Kanuni na nyaraka mbalimbali za elimu.
  • Kuandaa, kusambaza na kutumia taarifa na takwimu za shule kwa wakati na zikiwa sahihi.
  • Kukusanya na kusimamia mapato na matumizi ya fedha za shule kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
  • Kuandaa, kusimamia na kuendesha mafunzo ya ndani kwa walimu ikiwa ni pamoja na kutoa “orientation” kwa walimu wapya.
  • Kusimamia ustawi wa walimu na wanafunzi ili kila mmoja awajibike na apate haki zake zote kadri inavyowezekana.
  • Kuandaa wa jumla wa shule na mpango wa maendeleo, mpango wa kazi na kuwasilisha ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata na Halmashauri.
  • Kuwa kiungo kati ya shule na jamii pana.
  • Kuwa Katibu wa vikao vya Bodi ya Shule na kuhakikisha inakuwa hai wakati wote. Bodi huwa na vikao vya kawaida
  •  visivyopungua vine. Bodi ndicho chombo kikuu cha kumsaidia Mkuu wa Shule kuendesha shule.
  • Kufundisha masomo aliyosomea ili kuwa mfano (model) na kuimarisha ualimu wa Mkuu wa Shule.
  • Kusimamia na kudumisha nidhamu kwa wanafunzi na maadili kwa walimu ili kurejesha heshima ya ualimu.
  • Kuboresha mazingira ya shule ikiwa ni pamoja na kuyajanisha na kutengeneza viunga.
  • Kusimamia ukarabati wa miundombinu ya shule yakiwemo majengo na madawati ili yawe katika hali bora wakati wote.


HALMASHAURI YA MJI WA BABATI
MPANGO KAZI ELIMU TAALUMA  SEKONDARI 2024/2025
S/N MALENGO MAKUU MALENGO MAHSUSI MAHITAJI MUDA WA UTEKELEZAJI WAHUSIKA MATOKEO
1 Kufuatilia ufundishaji na Ujifunzaji katika shule 21 za sekondari Kufanya ufuatiliaji wa ufundishaji na ujifunzaji, ratiba kuu ya masomo na mahudhurio ya walimu kazini. Magari, Mafuta, rimu za karatasi  na wino wa printer. Januari-Disemba TSEO,TSAO, TSSEO,TSAEO,SLOS, H/M, WEOS, Walimu Zoezi la ufundishaji na ujifunzaji shuleni kufanyika kwa kufuata taratibu,Kanuni na Sheria za Kazi
2 Kubuni mipango ya Kuinua kiwango cha  Taaluma katika Halmashauri na kusimamia utekelezaji wake Vikao vya Maafisa Elimu Kata wakuu wa shule na Walimu wa Taaluma, Karatasi na wino wa printer  Febuari  TSEO,TSAO, H/M,WEOS, Walimu wa Taaluma Makubalino tuliyojiwekea kutekelezwa na ubora wa matokeo kuonekana
Kuandaa na Kufanya Semina  za walimu wa Masomo Fedha, Chakula, Karatasi na wino wa printer  Febuari - March TSEO, TSAO, H/M, WEOS Wawezeshaji walimu waliotoka Marking, Walimu  Walimu kuelewa utunzi wa Mitihani kwa kutumia umahiri (competence base) na namna mitihani ya Taifa inavyotakiwa kujibiwa
3 Kuratibu shughuli za ufanyikaji wa Mitihani ya ndani ya shule na Mitihani ya Taifa  Kufanya usajili wa watahiniwa wa kidato cha Pili, cha Nne na kidato cha Sita Karatasi na wino wa printer  Octoba - March TSEO,TSAO, H/M, Walimu wa Usajili Kupata idadi kamili ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa Taifa kidato cha Pili (FTNA), Nne (CSEE) na Kidato cha Sita (ACSEE) Kwenye CAL, ISAL na PHOTOENTRY
 Kuandaa na Kufanya Mitihani ya ndani Pre-Mock Halmashauri, Mock Halmasahuri na Mkoa ikiwa ni utunzi, uzalishaji, kusambaza  kusahihisha , kutoa matokeo  Pamoja na Kufanya Tathmini Fedha, Printer, Wino, Karatasi,gari, mafuta,Mfumo wa kuchakatia matokeo May, Julay, September TSEO,TSAO, H/M,WEOS,Walimu, Walimu wa Taaluma Mtihani wa utamirifu Kidato cha Pili, Nne na Kidato cha Sita  kufanyika, kupata matokeo  kubaini shule bora na duni na kuzifanyia ufuatiliaji.
Kuandaa majina ya Wasimamizi wa Mitihani ya Taifa  na kuyapeleka katika vyombo vya upekuzi Karatasi na wino wa printer  Machi, Julay, Agosti Kamati ya Mitihani, H/M,WEOS, DSO, RAS Kupata orodha ya majina ya walimu wenye sifa  watakaosimamia Mtihani ya Taifa FTNA, SCEE, ASCEE

Kuratibu shughuli za ufanyikaji wa Mitihani ya ndani ya shule na Mitihani ya Taifa  Kuandaa mapendekezo ya bajeti ya Upimaji wa Taifa kidato cha Pili, Nne na Kidato cha Sita  Fedha, Chakula, Karatasi na wino  printer na Mwongozo wa Malipo  Agosti - Novemba, Octoba Kamati ya Mitihani ya Mitihani  Kupata bajeti/kiasi cha fedha zinazohitajika katika uendeshaji wa Mtihani ya Taifa FTNA, SCEE, ASCEE
Kuratibu zoezi zima la ufanyikaji wa Mitihani ya Taifa  Magari, mafuta Posho,  May, October, November Kamati ya Mitihani ya Mitihani  Mitihani kufanyika katika hali ya usalama
Kufanya Tathmini ya Matokeo ya Mitihani ya Pre-Mock Halmashauri,Mock Halmasahuri na Mkoa Pamoja na Mitihani ya Taifa kidato cha Nne Karatasi na wino wa printer, Gari, Mafuta, Fedha Januari, April, Julay TSEO,TSAO, H/M,WEOS, Walimu wa Taaluma Kupata idadi kamili ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa Taifa PSLE 2023 (M1 na M3)
 Kuratibu na kusimamia utunzi wa mitihani ya kufunga mihula wa Pili kwa wanafunzi kidato cha Tatu na Kwanza.ikiwa ni utunzi, uzalishaji, kusambaza  kusahihisha , kutoa matokeo  Pamoja na Kufanya Tathmini Fedha, Printer, Wino, Karatasi,gari, mafuta,Mfumo wa kuchakatia matokeo Octoba - November TSEO,TSAO, H/M,WEOS, Walimu wa Taaluma, walimu Uwepo wa mitihani ya pamoja kwa shule zote ya kufunga muhula wa Pili kwa wanafunzi kidato cha Tatu na Kwanza..
4 Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule za Sekondari Kusoma taarifa za ukaguzi wa shule na kuwataka Wakuu wa Shule kujibu na kutekelezaji hoja na maelekezo yaliyotolewa na Wathibiti Ubora wa Shule Karatasi na wino wa printer, Gari, Mafuta Januari-Disemba TSEO,TSAO, TSSEO,TSAEO,SLOS,   Hoja za ukaguzi wa shule na maelekezo kufanyiwa kazi na kujibiwa kwa wakati. Pia shule zilizobainika kuwa na mapungufu makubwa kufanyiwa  ufuatiliaji wa mara kwa mara.
5 Kuratibu utoaji wa huduma Mbalimbali kwa wanafunzi, Walimu na Watumishi wasio walimu  Kufanya ufuatiliaji  na kuhakikisha  utoaji huduma muhimu kwa wanafunzi, walimu na watumishi wengine zinapatikana mfano mahudurio ya walimu na wanafunzi, uhamisho wa wanafunzi ndani na nje ya Halmashauri, Utoaji wa chakula shuleni Gari na mafuta,        Kuingia kwenye mfumo wa PReM Januri hadi Disemba TSEO,TSAO, TSSEO,TSAEO,SLOS, H/M, WEOS, Walimu Wanafuzi kuweza kuhama kutoka shule moja kwenda nyingine, Pamoja nakupata chakula cha Mchana.
6 Kubaini na  Kuratibu mafunzo  ya walimu kazini na watumishi wengine wa shule za sekondari Kuanda orodha ya walimu walioomba kuwekwa kwenye mpango wa mafunzo 2024/2025 Karatasi na wino wa printer Januari Agosti-Novemba TSEO,TSAO,  Walimu kupewa ruhusa za kwenda masomoni kujiendeleza.
7 Kuratibu Mashindano ya michezo na taaluma ya shule za Sekondari katika Halmashauri  Kuratibu zoezi zima la michezo kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi Taifa. Magari, mafuta, rimu za karatasi  wino wa printer. Fedha March- Juni TSEO,TSAO,  Wanafuzi kuweza kushiriki michezo
8 Kuratibu, kukusanya na kuchambua takwimu za elimu ya sekondari katika Halmashauri Kupata Idadi ya wanafunzi  walioripoti kidato cha kwanza na cha Tano 2024/2025, Kuwa na takwimu za walimu wote shuleni, miundombinu ya shule na samani Karatasi na wino wa printer computer  Januari -Machi SLO (S), TSEOS,TAOS,TSSNEO,TSAEO Takwimu zimekusanya na zinatumika
Kuandaa takwimu za Elimu za mwaka(ASC-Annual School Census) Karatasi na wino wa printer Aprill -June SLO (S), TSEOS,TAOS,TSSNEO,TSAEO Takwimu zimekusanya na zipo kwenye mfumo ANS
9 Kusimamia na kufuatilia ukarabati, upanuzi na ujenzi wa shule za sekondari Kuwa na takwimu zinazoonesha mahitaji ya ujenzi wa shule kikata, kuandaa orodha ya maboma ya miundombinu kwa ajili ya umaliziaji, kuhakikisha ujenzi wote unaoendelea unakamilika kwa wakati. Usafiri, karatasi, wino, printer Januari- Disemba SLO (S), TSEOS,TAOS,TSSNEO,TSAEO Takwimu zinazoonesha mahitaji ya ujenzi wa shule zinatumika kwenye kuainisha maeneo yenye mahitaji ya ujenzi
10 Kukisia mahitaji ya walimu kimadaraja na kimasomo kulingana na Ikama Kuhakikisha Ikama ya walimu katika shule za serikali imekaa vizuri. Shule zote ziwe na uwiano unaolingana wa walimu na wanafunzi kimasomo Usafiri, karatasi, wino, printer Januari- Disemba SLO (S), TSEOS,TAOS,TSSNEO,TSAEO Ikama ya walimu inazingatiwa na walimu wanapangwa kwa uwiano mzuri
11 Kuagiza na kusambaza vifaa vya shule kufuatana na mahitaji ya shule Kuhakikisha kuwa shule zote za sekondari za serikali zina vifaa vyote vinavyohitajika kwa uwiano mzuri kwa ajili ya ufundishaji na ujifunzaji Usafiri, karatasi, wino, printer Januari- Disemba SLO (S), TSEOS,TAOS,TSSNEO,TSAEO Vifaa vyote vilivyoagizwa vimesambazwa kwa uwiano mzuri
12 Kufuatilia mapato na matumizi ya fedha katika shule za sekondari Kuhakikisha shule zinapata fedha za Elimu Bure kulingana na mwongozo,kusimamia uandaaji na utunzaji wa taarifa za mapato na matumizi. Kuhakikisha matumizi ya fedha yanafuata mwongozi. Usafiri, karatasi, wino, printer Januari- Disemba SLO (S), TSEOS,TAOS,TSSNEO,TSAEO Matumizi ya fedha za shule zinatumika kulingana na miongozo ya fedha.
13 Kuratibu utoaji  Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi katika Halmashauri. Kusimamia utekelezaji wa mipango ya EWW na ENMRA katika vituo vinavyotoa Program za MEMKWA, MUKEJA na Maswala Mtambuka kwa kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na mashirika binafsi.  Magari, mafuta, rimu za karatasi  na wino wa printer. Juni -July TSEO, TSAEO,TCDO, IAE Zoezi la utekelezaji wa program za Elimu ya Watu wazima  kufanyika kwa kufuata utaratibu mzuri
14 Kuandaa bajeti ya Elimu ya Watu wazima na Elimu Nje ya Mfumo rasmi Kuandaa makisio ya mahitaji ya EWW na ENMRA kwa ajili ya kuweka kwenye bajeti ya Elimu Sekondari karatasi wino wa printa Disemba - March TSEO, TSAEO, kuwepo kwa rasilimali kwa ajili ya uendeshaji wa EWW
15 Kuratibu na kusimamia zoezi la utoaji wa mafunzo kwa walimu (MEWAKA) Kutembelea shuleni na vituo vya walimu ili kuhamasisha utoaji wa mafunzo endelevu kazini kwa walimu Magari, mafuta, rimu za karatasi  na wino wa printer. Julai-Juni  TSEO, TSAEO, TSAO Walimu kuboresha ufundishaji na ujifunzaji
16 Kukusanya, Kuchanganua na kutayarisha Taarifa za utekelezaji wa Elimu ya watu wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Katika Halmashauri. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa programu za EWW na ENMRA  za  robo, na za mwaka Karatasi compyuta Printer Julai-Juni  TSEO, TSAEO,  Uwepo wa taarifa za kila robo na ya mwaka
17 Kupitisha na kukokotoa maombi ya likizo za walimu  kupitisha fomu za likizo na kukokotoa maombi ya fedha za nauli kwa walimu wanaostahili malipo.  Rimu za karatasi  na wino wa printer. April ,May, Agosti , September TSEO, TSAEO,  Walimu wanaostahili kwenda likizo kupata stahiki zao mapema.
18 Kuratibu na kusimamia maadhimisho ya juma la Elimu ya Watu Wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi Kuratibu na kusimamia maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima kikata na Kihalmashauri. Magari, mafuta, rimu za karatasi  na wino wa printer. Agosti TSEO, TSAEO,  Maadhimisho ya Juma la Elimu kufanyika
19 Kufuatilia,Kusimamia na Kutathimini taarifa za maendeleo ya utoaji elimu maalum katika shule za sekondari Halmashauri  Kufuatilia hali ya utoaji wa elimu maalum katika shule za sekondari kuanzia kidato cha I hadi cha VI Gari,Karatasi na wino wa printer  Januari -Machi TEOS NA TSSNEO Kupata idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule zote za sekondari.
Kutoa taarifa ya wanafunzi wenye ulemavu wanaostahili kufanya mtihani wa kidato cha II kwa Afisa taaluma sekondari Karatasi na wino wa printer Januari -Machi TEOS NA TSSNEO Kupata idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaotarajiwa kufanya mtihani wa upimaji kidato cha pili 
Kupata idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaotarajiwa kufanya mtihani wa upimaji kidato cha Nne  Karatasi na wino wa printer Januari-Machi TEOS,TSSNEO NA TAOS Kutoa taarifa ya wanafunzi wenye ulemavu wanaostahili kufanya mtihani wa kidato cha IV kwa Afisa taaluma sekondari
20 Kukusanya,Kuchangunua,Kutunza na Kutoa takwimu sahihi zinazohusu Elimu Maalum Kupata takwimu sahihi ya vituo vya Elimu maalum,Walimu,Wanafunzi na vitendea kazi katika vituo vya elimu maalum Magari, mafuta, rimu za karatasi A4  na wino wa printer. Januari -Machi TEOS,TSSNEO NA SLO Kupata idadi sahihi ya vituo,walimu,wanafunzi na vitendea kazi katika vituo vya kutolea elimu maalum ili kurahisisha utoaji wa elimu kwa wenye uhitaji wa elimu maalum
21 Kuratibu utoaji wa elimu maalum katika elimu ya Sekondari,Elimu ya Watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi Kuandaa taarifa ya utoaji wa elimu maalum katika elimu ya Sekondari,Elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi Karatasi na wino wa printer Aprili-Mei TEOS,TSSNEO NA TSAEO Kupata  orodha sahihi ya shule za sekondari,Vituo vya Elimu ya Watu wazima na vituo vya shule nje ya mfumo rasmi vyenye wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Kuandaa  orodha ya majina ya walimu wanaofundisha elimu maalum katika Sekondari,Elimu ya Watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi Orodha ya majina ya walimu wote wa shule za serikali Mei -Juni TEOS,TSSNEO NA TSAEO Kupata orodha ya majina ya walimu wanaofundisha elimu maalum katika mfumo rasmi na nje ya mfumo rasmi
Kufanya uchambuzi wa matokeo ya mitihani ya muhula wa kwanza kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum Walimu,Karatasi,Wino na Printer  Julai TEOS,TSSNEO NA TSAEO Kuandaa taarifa ya matokeo ya mitihani ya muhula wa kwanza kwa wakati
22 Kuratibu utoaji wa huduma muhimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum Kupokea taarifa za uendeshaji wa vituo vya Elimu maalum katika utoaji wa huduma muhimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum Karatasi na wino wa printer Agosti-Novemba TEOS NA TSSNEO Kupatikana kwa  taarifa za huduma muhimu zinazotolewa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa wakati
Kutembelea vituo na shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum gari na mafuta Agosti-Novemba TEOS NA TSSNEO Kutolea taarifa mapungufu na changamoto za vitu vya elimu maaluma na kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo
23 Kuandaa bajeti ya elimu maalum kulingana na mahitaji ya kila shule maalum,Shule jumuishi na vitengo vya elimu maalum Uchambuzi wa majeti ya vituo vya utoaji wa elimu maalum  Karatasi na wino wa printer Novemba-Desemba TEOS,TSSNEO,TAOS NA SLO Kuwasilisha bajeti ya elimu maalum kwa wakati
24 Kufanya kazi nyingine zitakazojitokeza,tutakazoagizwa na Afisa Elimu au Mkurugenzi

Januari-Desemba


HALI YA TAALUMA
MIKAKATI YA KUBORESHA TAALUMA KWA MWAKA 2021
CHANGAMOTO
UTATUZI WA CHANGAMOTO


Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili 2025. May 08, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR CONSTRUCTION SUPERVISION CONSUTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BABATI TOWN UNDER TACTIC PRJECT TIER 2 March 07, 2025
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI 2025. May 13, 2025
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI 2025. May 13, 2025
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Kikao kazi cha maazimio ya mikakati ya kupunguza Ukatili wa kijinsia.

    May 29, 2025
  • Wakazi wa Halmashauri ya Mji Babati wanufaika na Gulio la Gendi.

    May 28, 2025
  • Elimu ya Matumizi sahihi ya Dawa za Binadamu imetolewa kwa Watumishi wa Halmashauri ya Mji Babati.

    May 28, 2025
  • Baraza maalum la Hoja Halmashauri ya Mji wa Babati.

    May 27, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Babati 2024
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati