Ugawaji wa Vitambulisho kwa baadhi ya wajasiriamali wadogo wadogo Mjini Babati
Nawapongeza sana kwa kitendo cha kizalendo kumuunga mkono mheshimiwa Rais kwa kuweza kuchangia sh. 20,000 kwa ajili ya vitambulisho ambazo kwa kweli nina imani kubwa zimefanya maendeleo katika taifa letu la Tanzania.
Nawapongeza sana wamachinga na wajasiriamali wadogo wadogo wote kwa umoja wenu na shughuli zenu za ujasiriamali kwani mmefanya mji wetu wa Babati kuchangamka na kurahisisha upatikanaji wa Bidhaa na mahitaji mbalimbali kwa wananchi, hivyo mimi rai yangu kwenu sasa na mwaka huu tuchangie hiyo elfu ishirini (20,000) kama jinsi serikali yetu ilivyotuomba na kutuagiza tununue na tusisumbuliwe katika kutoa au kulipa kodi nyingine yoyote, hiyo elfu ishirini inatosha. amesema mheshimiwa mkuu wa Wilaya.
Kwa picha zaidi bonyeza kituo cha habari kwenye menyu.
Imeandikwa na Nyeneu, P. R
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati