Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Babati Mjini kwa kuzingatia kanuni ya 14 ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020 na kanuni ya 12 ya kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa (Uchaguzi wa madiwani) za mwaka 2020 anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za watendaji wa Uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.