Ziara ya mafunzo kwa waheshimiwa madiwani, wakuu wa Idara na Vitengo walipotembelea Halmashauri ya Mji wa Geita. Mambo ambayo Waheshimiwa Madiwani na wakuu wa Idara na Vitengo walitakiwa kujifunza ni pamoja na Utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa fedha za ruzuku, mapato ya ndani na fedha za wafadhili. Gharama za ujenzi wa miradi ya Kimkakati (Mapato, Usafi wa mazingira), Namna miradi ya kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani (Own Source Revenue). Aidha waheshimiwa madiwani na wataalam walitembelea miradi mbalimbali wakibadilishana uzoefu wa namna tofauti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Babati Bw. Faustine Masunga akitoa utambulisho mfupi kwa wataalamu waliotembelea Halmashauri ya Mji wa Geita.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati