Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji, Mitaa pamoja na Wajumbe Halmashauri ya Mji wa Babati wamepewa mafunzo yenye kuwajenga katika kutekeleza majukumu yao ya kuwatumikia Wananchi. Viongozi takribani 535 kwa Kata zote wamepewa mafunzo hayo katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Babati day .
Mafunzo hayo yamejumuisha wawezeshaji mbalimbali wakiwemo Maafisa kutoka TAKUKURU(Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa, Jeshi la Polisi, Jeshi la Uhamiaji , Wakuu wa Idara na Maafisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuella Kaganda ameeleza kuwa mafunzo haya yanalenga kuwajenga Viongozi kutambua wajibu wao, kutambua muundo wa Utawala na kutambua mambo ambayo hawatakiwi kufanya kama Viongozi.
Aidha Mhe. Kaganda amewapongeza na amewataka Viongozi hao waliochaguliwa kutimiza wajibu wao kwa haki,kusimamia usalama na amani katika maeneo yao na kuwasaidia Wananchi kupata maendeleo.
Sambamba na hilo Mrakibu kutoka Jeshi la Polisi Bw.Emmanuel Kandola amewataka Wenyeviti kujiepusha na tamaa ndogo ndogo zinazopelekea migogoro ya Ardhi katika maeneo yao ambapo hupelekea Wananchi kukosa Imani na Serikali yao .
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati