Wenyeviti na wajumbe wa kamati za Mitaa, vijiji,na vitongoji kundi mchanganyiko na kundi la Wanawake katika Halmashauri ya Mji wa Babati walioshinda kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27/11/2024 wameapishwa rasmi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao.
Uapisho huo umefanyika tarehe 28/112024 katika Halmashauri ya Mji wa Babati mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Jumaa Mwangome Mwambago.
Msimamizi wa Uchaguzi CPA. Shaaban Mpendu amewapongeza kwa kuaminiwa na Wananchi, na amewataka wakawatumikie Wananchi kwa uaminifu na uadilifu kwa kuwa ndio kazi ya Uongozi,
“Hongereni sana kwa kuteuliwa mkawasaidie Wananchi kupata maendeleo”alisema Mpendu.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati