• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Biashara
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Waziri Lukuvi Azindua Ofisi za Ardhi Mkoa wa Manyara: Agawa hati

Imechapishwa: June 24th, 2020

Waziri wa ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. WILLIAM VANGIMEMBE LUKUVI akiwa mjini Babati amezindua ofisi za Ardhi mkoa wa Manyara jana tarehe 23 Juni 2020 ikiwa katika kuhitimisha utekelezaji maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kupunguza na kuondoa kabisa migogoro ya Ardhi katika maeneo mbalimbali ya Tanzania. 

Leo nimekuja kuhitimisha maagizo ya mhe. Rais, Aliponiteua aliniambia kazi kubwa ya kuifanya ni kuondoa migogoro. Alisema Waziri

Akiongea na viongozi, watumishi na wananchi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo, amesema migogoro ya Ardhi katika nchi yetu ilikuwa imetamalaki sana kipindi cha nyuma. Ameongeza na kusema kuwa katika kutekelezaji huo Wizara ya Ardhi imejitahidi sana kupunguza migogoro ya kiutawala mijini kwa namna ya kuonana na wananchi, wizara imeweza kutatua migogoro zaidi ya elfu kumi na mia tano (10,500). Pia aliongeza kuwa, kwa kutumia mabaraza ya Ardhi na nyumba Wizara imeweza kutatua migogoro zaidi ya laki tatu, ambayo yote haya yamefanyika katika kipindi hiki cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano.

Katika kufanikisha yote hayo, Wizara ya Ardhi kupitia maagizo ya Rais, imeweza kuondoa mfumo wa urasimu katika kumiliki Ardhi. mfumo huu wa kiurasimu ulikuwa haumuwezeshi mwananchi wa kawaida kuweza kumiliki Ardhi kutokana na gharama kubwa zilizojificha na ambazo sio za kisheria.

Gharama za umilikishaji kisheria ni ndogo sana ukilinganisha na gharama ambazo zilikuwa hazisemwi wananchi ambao walikuwa wanazigharamia kwenda kupata haki yake ili akamirishe umiliki. Aliongeza mhe. Waziri.

Mhe. Waziri amelaani kitendo cha baadhi ya watumishi maofisini kuwanyanyasa wananchi ambao tayari wameshapimiwa maeneo yao na wameshalipa gharama zote kwenye Halmashauri husika za umilikishaji, na hati zao zikiwa tayari zimeshatiwa sahihi kuambiwa kuwa walipe nauli na gharama zingine za maisha ili hati zao zifuatwe moshi ambapo zamani ilikuwa ndo mahali hati zilikuwa zinatolewa kwa kanda ya kaskazini, amesema huo ni utumwa na umekomeshwa mara moja.

Sasa wale wananchi waliopimiwa na wameshalipa gharama zote kwenye halmashauri za umilikishaji, na hati wameshatia sahihi wanaambiwa wao wenyewe tena walipe nauli na gharama zingine za maisha wafaute hati moshi, huo ni utumwa. Alizidi kusisitiza mhe. Waziri

Aidha, katika uzinduzi wa ofisi hizi za mkoa, mhe. Waziri amegawa hati kwa watu, watu ambao hati zao zilikuwa tayari zimetayarishwa kutoka Babati na kusainiwa na kusajiliwa na kamishani hapa hapa Babati, hii ikiwa ni kuashiria kuwa ofisi hizi zimezinduliwa na tayari zimeanza kazi.

Sambamba na hilo, mhe. mkuu wa Mkoa wa Manyara Ndg. Alexander Mnyeti aliipongeza Idara ya Ardhi kuwa wako vizuri na wameanza vizuri na kazi yao ni nzuri. Mhe. mkuu wa Mkoa alimueleza Waziri kuwa hapo zamani Mkoa wa Manyara ulikuwa umekumbwa na migogoro na kesi za Ardhi. Lakini tangu uteuzi wa viongozi mbalimbali kwenye hizi ofisi mpya za Ardhi mkoa, mambo yamekuwa ni mazuri kwani hakuna malalamiko yoyote. Mhe. mkuu wa Mkoa aliendelea kwa kuelezea kero mbalimbali za Ardhi zilizopo katika mkoa wa Manyara na kusema kuwa kesi hizi zimekuwa ni changamoto sana kiasi kwamba kupelekea kuathiri shughuli zingine za kijamii.

Kwahiyo ukiamka ni Ardhi, ukilala ni Ardhi na kwa bahati mbaya sana kila kitu kinafanyika kwenye Ardhi basi kila kitu kimekuwa ni Ardhi. Na watu wetu huku wanapenda Ardhi na wanapenda pia migogoro. Alisema mkuu wa Mkoa. 

Aidha, mhe. Mkuu wa Mkoa alimpongeza mhe. mkuu wa Wilaya ya Kiteto kwa uongozi ulioimara kwani ameweza kudhibiti matukio ya mauaji ambayo hapo nyuma yalikuwa ni ya kila siku. Kuwa kwa sasa wote ni mashahidi kwa miaka minne mfululizo katika uongozi wa Mkuu wa Wilaya, hakuna tukio la mauaji lililosikika, hii ikiwa ni kwa sababu ya uongozi imara.

Mhe. Mkuu wa Mkoa amekemea vikali kitendo cha baadhi ya watu kumiliki maeneo makubwa ya Ardhi na pasipo kuyaendeleza wakati huo huo kuna wananchi wa kawaida ambao wanahitaji maeneo kwaajili ya kilimo na mifugo na pia wawekezaji wengine wanataka maeneo kwaajili ya uwekezaji. Ndg Mnyeti alimalizia kwa kumuomba Mhe. Waziri kuwa mashamba na maeneo kama haya ambayo yanakaa muda mrefu bila kuendelezwa na ni mapori, apewe muwekezaji mwingine na kama hapatikani, basi yarudishwe kwa wananchi.

Naye Kamishna msaidizi wa Ardhi mkoa wa Manyara, Ndg. Leonard Msafiri alisoma taarifa ya sekta ya Ardhi mkoa wa Manyara mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Lukuvi katika uzinduzi wa ofisi za Ardhi mkoa wa Manyara. Katika taarifa hiyo, Ndg Leonard alisema kuwa ofisi ya Ardhi mkoa wa Manyara ni mojawapo ya ofisi 26 za wizara ya Ardhi Tanzania Bara zilizoanzishwa kwa lengo la kusogeza huduma za wizara kwa wananchi, ambapo ofisi hii ilianza kazi mwanzoni mwa Mwezi Machi 2020 na hadi sasa ofisi ina watumishi 18 ambao wamehamishiwa kufanya kazi ofisi za Ardhi mkoa wa Manyara na tayari wameripoti wote na wanaendelea kutekeleza majukumu yao. Aliendelea kwa kutoa shukrani za dhati kutoka katika uongozi wa Mkoa wa Manyara kwa mhe. Waziri kwa kutoa pendekezo la kugatua madaraka katika usimamizi wa Ardhi katika ngazi za mikoa na mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kuridhia na kufanya uamuzi wa kupeleka huduma za Ardhi zilizokuwa zinatolewa na Wizara katika ngazi za mikoa.


Imeandikwa na Nyeneu, P. R

Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR CONSTRUCTION SUPERVISION CONSUTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BABATI TOWN UNDER TACTIC PRJECT TIER 2 March 07, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili 2025. May 08, 2025
  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Mji Babati imefanya Ziara kukagua Miradi ya Maendeleo

    May 07, 2025
  • Watumishi Manyara wametakiwa kupendana na kuacha chuki.

    April 30, 2025
  • Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amewataka Wananchi kuuenzi Muungano.

    April 26, 2025
  • Chanjo nyongeza ya polio (IPV2) kuanza kutolewa kwa watoto wa miezi 9 mwezi wa tano 2025.

    April 24, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Babati 2024
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati