Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Babati wamefanya bonanza la michezo na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kutoka Mkoani Dodoma ambapo kumekuwa na mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Mkoani Manyara.
Katika bonanza hilo Timu ya mpira wa pete ya Halmashauri ya Mji wa Babati imeibuka kidedea baada ya kuifunga magoli 55-4 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na katika mpira wa miguu Timu zote mbili zimetoka sare ya magoli 5-5.
Afisa Michezo,Sanaa na Utamaduni Halmashauri ya Mji wa Babati Bw.Jumaa Kifula amewapongeza washiriki wa timu zote mbili na amewakaribisha sana Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.
Pia ameongeza kuwa wataandaa safari ya kwenda Chemba kwa ajili ya kushiriki Bonanza watakalo liandaa Watumishi wa Chemba,michezo ni afya, huleta ushirikiano na umoja baina ya Watumishi hivyo wapo tayari kwa mwaliko huo.
Vilevile Kaimu Afisa Michezo,Sanaa na Utamaduni kutoka Chemba amesema kuwa wamejifunza vingi kutoka kwa Watumishi wa Babati na amewakaribisha sana Chemba kushiriki katika bonanza la michezo na ameongeza kuwa michezo ni furaha imependeza kushiriki katika michezo hiyo.
KAULI MBIU ''Michezo nia Afya na huleta undugu na mshikamano''
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati