Maafisa Biashara Halmashauri ya Mji wa Babati wametoa mafunzo ya Mfumo wa Ukusanyaji wa mapato(TAUSI PORTAL) kwa Watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara.
Mafunzo hayo yanalenga kuongeza ufanisi zaidi katika kukusanya mapato Halmashauri ya Mji wa Babati,pia wamepewa mafunzo ya utoaji wa leseni ya biashara na leseni ya vileo katika mtandao ili kuwawezesha kusaidia na kupunguza idadi kubwa wateja kufika Ofisini,wananchi anaweza kujihudumia mwenyewe.
Pia katika mafunzo hayo wamefanya mapitio ya Sheria ya leseni za Biashara Sura Na.25 Mwaka 1972 pamoja na marekebisho yake.Vilevile wamepewa mafunzo katika ukusanyaji wa Ushuru wa Huduma(Service Levy) na namna ya kukagua leseni za ubora wa vyakula.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati