Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji wa kata zote nane za Halmashauri ya Mji wa Babati wamepewa mafunzo ya kuwakumbusha maelekezo mbali mbali ya kiutumishi yakiwemo masuala ya maadili ya utumishi wa umma,stahiki kwa watumishi wa umma Pamoja na makosa yanayoweza pelekea Mtumishi kuchukuliwa hatua za kisheria kwenye utumishi wa Umma, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA. Shaaban Mpendu amewakumbusha kuwa watendaji wanatakiwa kuhakikisha usalama amani na utulivu unadumishwa katika maeneo ya makazi,kushughulikia kero za wananchi Pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mipango na bajeti.
Aidha mkuu wa dawati la kuzuia Rushwa Bw. Pascal Mhalawa kutoka TAKUKURU(Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa) ameelezea namna Rushwa inavyoweza kujitokeza katika mazingira ya kazi, wakati wa kutafuta kazi, watumishi wanawake wanavyoweza kutengenezewa mazingira ya Rushwa. Pia amewataka watendaji kujiepusha na vitendo vya Rushwa.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati