Wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Babati wamepewa Mafunzo ya Mfumo wa N-Card.
Mafunzo hayo yamewezeshwa na Kituo Cha kuhifadhi data kwa njia ya Mtandao(National internet data centre 'N-Card) na kufanyika katika Ukumbi wa White Rose.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo muwezeshaji Bw.Abdalah Mfundo ameeleza kuwa matumizi ya N- Card yameweza kurahisisha malipo kwaTaasisi za Serikali pamoja na kukusanya mapato halisi.
Pia ameeleza kuwa Mfumo wa N-card umeweza kutumika katika Taasisi mbalimbali kama Damu salama, Stendi ya Magufuli,Temesa,Puma, Uwanja wa Mkapa na Viwanja vya michezo nchini Tanzania ukiwemo uwanja wa Tanzanite Kwaraa na kuleta matokeo chanya .
Aidha ameeleza kuwa Kituo Cha kuhifadhi data kwa njia ya mtandao kinakusudia kuendelea kuongeza wigo wa kiutendaji kwa kushirikiana na Serikali kwa maridhiano ya ukusanyaji wa mapato katika shughuli mbalimbali.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati