Watumishi Pamoja na Waratibu wa mfumo wa e -mrejesho kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara wamepewa mafunzo ya siku tatu juu ya namna ya kutumia mfumo wa e-mrejesho utakaosaidia watumishi na Wananchi wa kawaida kutuma mrejesho wa malalamiko, pongezi,mapendekezo na maulizo ili kushughulikia kero mbali mbali za Wananchi na Watumishi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kaimu Mkurugenzi ofisi ya Rais Menenjimenti ya utumishi wa umma na utawala Bora Bw. Ally Ngowo ameeleza kuwa dhana ya e mrejesho imelenga kuimarisha Utawala Bora, kujenga uhusiano wa karibu kati ya Wananchi na utumishi wa Umma Pamoja na kuimarisha uwajibikaji kwa watumishi.
Aidha amewataka washiriki wote kuhakisha wanaandaa mpango kazi wa kuwajengea uwezo watumishi kutuma mrejesho katika maeneo yao ya kazi ili watu wote waelewe namna ya kutumia mfumo katika kutoa mrejesho Pamoja na kuhakikisha ofisi za waratibu mrejesho zinafikika kwa urahisi PIa kuweka masanduku ya maoni .
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati