Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Jimbo la Babati Mjini limeendelea katika Vituo vyote 64 katika Mitaa na Kata Mkoa wa Manyara ambapo zoezi hilo ni kuanzia tarehe 04/09/2024 mpaka 10/09/2024 Kwa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Afisa mwandikishaji wa Jimbo la Babati Mjini Bi.Edna Moshi amewataka Viongozi wa Vyama vya Siasa kuwahamasisha wananchi wa Jimbo la Babati Mjini kuendelea kujitokeza kwenye Vituo vya Kujiandikisha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili wasiweze kupoteza haki yao ya msingi ya kupiga kura katika Uchaguzi wa Mwaka 2025.
Pia mawakala wa Vyama vya Siasa kwenye moja ya Kituo wamewaomba wananchi kujitokeza mapema kujiandikisha kwenye Daftari wakati huu na uandikishaji hautumii muda mrefu ni muda mfupi tu wanakwenda kuendelea na majukumu yao ya kila siku hivyo waendelee kujitokeza kujiandikisha
.
Vilevile Mwandishi Msaidizi wa Mtaa wa Bonga Mjini Kituo cha Shule ya Msingi Bonga Bw. Herman Samani ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza sasa wakati muda bado upo wasisubiri wakati wa siku zinapokuwa zimebaki chache katika Kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Vituo vilivyopo karibu na makazi yao.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati