Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bw.Bashan Kinyunyu kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi amefungua mafunzo kwa waandikishaji wapiga kura katika daftari la wapiga kura mkazi ambao watashiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Bw.Bashan amesisitiza uaminifu na kuzingatia maadili wameaminiwa kuteuliwa katika zoezi hilo hviyo wametakiwa kufanya kazi ya uandikishaji kwa weledi zaidi katika vituo vya kuandikisha wapiga kura wanaostahili kuandikishwa.
Aidha Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bi Edna Moshi amesisitiza suala la utunzaji wa siri katika zoezi hilo na ameongeza kuwa muda wa kufungua vituo na kufunga umetakiwa kuzingatiwa sana wakati wa uandikishaji ili kuhakikisha hakutakuwa na wananchi yeyeote anayesahaulika au kuachwa katika zoezi hilo la uandikishaji.
Vilevile katika mafunzo hayo waandikishaji wapiga kura takribani 160 wamejifunza kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,mambo ya kuzingatia wakati wa uandikishaji,sifa za mgombea, sifa ya mpiga kura pamoja na nafasi za Uongozi zinazogombewa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia wametakiwa kuhakikisha mpiga kura anayeandikishwa awe na kitambulisho cha Urai,kupiga kura,leseni ya udereva au barua ya utambulisho kumtambulisha kuwa muhusika na wamekumbushwa kukabidhi daftari wakati wa siku za mwisho kwa msimamizi msaidizi wa Uchaguzi.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika tarehe 27/11/2024 katika Halmashauri ya Mji wa Babati kuna jumla ya Vituo 90 vya Uandikishaji wapiga kura na zoezi la uandikishaji litaanza tarehe 11/10/2024 hadi 20/11/2024.
Sambamba na hilo Waandikishaji wa daftari la wapiga kura wameapa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Bw.Jumaa Mwangome Mwambogo na amewasitiza kuwa waaminifu na kuwajibika katika zoezi hilo.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati