Afisa lishe wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi Namsifu Godson amefanya zoezi la usambazaji na ugawaji wa Vitamini A katika Kituo cha Afya Bonga, Mutuka na Zahanati za Nakwa, Malangi, Kiongozi, Halla na HImiti. Walengwa zaidi wa Vitamini A ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Vilevile aliwapatia wahudumu wa Afya idadi ya watoto wanaotakiwa kuwafikia ili kutekeleza lengo. Usambazaji wa vitamin A tayari kwa kuanza zoezi la mwezi wa Afya na Lishe kwa watoto chini ya miaka mitano katika Halmashauri ya Mji wa Babati.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati