Jimbo la Babati Mjini limeanza rasmi Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Kata 8 yenye Vituo 64 kuanzia Tarehe 04/09/2024 hadi 10/09/2024 katika Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo wananchi wamejitokeza katika zoezi hilo ili waweze kupata fursa ya kupata Kadi na kuwa mpiga kura katika Uchaguzi wa Mwaka 2025 Mkoani Manyara.
Zoezi hilo limewahusisha Raia wa Tanzania,Awe ametimiza umri wa Miaka 18 au zaidi,Awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa Sheria nyingine zilizotungwa na Bunge na wahusika wa Uboreshaji wa Daftari anayejiandikisha kwa mara ya Kwanza mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na hajawahi kujiandikisha kwenye Daftari,atakayetimiza Miaka 18 ifikapo Tarehe ya Uchaguzi Mkuu 2025 na kwa wananchi aliyehama Jimbo la Uchaguzi anatakiwa kuboresha na aliyepoteza kadi au kuharibika.
Aidha Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Babati Mjini amesema kuna changamoto ya mtandao lakini limeshughulikiwa na ameomba wananchi waendelee kujitokeza katika Vituo vya Uboreshaji wa Daftrai la Kudumu la Wapiga katika Jimbo la Babati kuanzia Saa 2:00 Asubuhi hadi Saa 12:00 Jioni.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati