Mkoa mkoa wa Manyara mhe. Charles Makongoro Nyerere siku ya jumanne tarehe 31 Agosti 2021 alifanya ziara katika Kijiji cha Malangi kilichopo kata ya Maisaka katika Halmashauri ya Mji wa Babati. Ziara hii ilihusisha utatuzi wa mgogoro baina ya Mwekezaji wa shamba la miwa Dudumela Estate na Wananchi. Mhe. Makongoro alifanya ziara hii kutokana na Shamba la mwekezaji kuchomwa moto ekari 50 na watu wasiojulikana. Akiwa katika ziara hiyo Wilayani Babati, Mhe, RC alitoa uamuzi kuhusiana na mgogoro huo ambao umedumu kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.
Aidha, Mhe. Makongoro alisema alikuwa ameshatuma wataalum kwenda kufuatilia mipaka ya Eneo linalomilikiwa na Dudumela Estate. Kutokana na ripoti ya wataalamu wa Ardhi ya kikao kilichopita, imefahamika kuwa Wananchi wanaoishi katika eneo ambalo mwekezaji anadai kuwa ni eneo lake wapo kimakosa na hatimilki zao ni batili (Hazitambuliki kisheria), hivyo mwekezaji ndo mmiliki halali wa eneo hilo.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati