Mafunzo ya Usambazaji na Matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 yamefanyika katika Halmashauri ya Mji wa Babati Ukumbi wa CCM Mkoa wa Manyara ambapo Mafunzo hayo yametolewa kwa Halmashauri zote mbili,Halmashauri ya Babati Vijijini na Halmashauri ya Babati Mjini ambapo mgeni Rasmi katika mafunzo hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Jacob Twange amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga katika ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yametolewa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) lengo ikiwa ni kuhamasisha matumizi ya matokeo ya Sensa katika Halmashauri hizo Serikali iko katika awamu ya tatu ya utoaji wa elimu na uchakataji wa ripoti za matokeo ya Sensa ambapo awamu iliyopo ni utoaji wa matokeo ya Sensa kwa makundi ya Viongozi na Wadau mbalimbali.
Katika utoaji wa taarifa fupi ya ufunguzi wa mafunzo hayo mtamkwimu wa Mkoa Bw. Gidion Mokiwa ameeleza kuwa matokeo ya Sensa ni tofauti na matokeo ya utafiti, matokeo ya Sensa hutoka kwa awamu sambamba na hilo mtakwimu huyo amewataka wadau wa maendeleo wanaohitaji matokeo kushirikiana na Ofisi ya Takwimu Mkoa ili kupata taarifa.
‘’Mipango bila takwimu ni suala gumu’’ Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Daniel Silo wakati akizugumza katika mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi 2022 yatasaidia kujuwa mapungufu yaliyopo katika Wilaya hiyo.Pia amewataka washiriki kutoa maoni katika dira ya Taifa 2050 kikamilifu ili kuleta ufanisi zaidi katika Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Babati amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha vizuri zoezi la Sensa ya watu na makazi mwaka 2022 vilevile ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Manyara takribani shilingi Bilioni 600.
‘’Mafunzo haya yataenda kuongeza ufanisi ili mambo yote yafanyike ndani ya Wilaya kwa kufuata matumizi ya matokeo ya sensa’’ Mhe. Tangwe amesema hayo katika ufunguzi wa mafunzo hayo pia amewataka kamati za maendeleo za Kata na Wilaya kuzingatia matumizi ya matokeo ya Sensa vilevile ameahidi Wilaya kushirikiana kikamilifu na Ofisi ya Takwimu.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati