• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Biashara
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi amshukuru Mhe. Rais Mbele ya Baraza la Madiwani Mjini Babati

Imechapishwa: December 11th, 2020

Imeandikwa na Nyeneu, P. R - Mjini Babati

Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Mbunge kutoka jimbo la Babati Mjini Mheshimiwa Pauline Philipo Gekul, tarehe 11 Novemba 2020 amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Joseph Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua kumsaidia Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mashimba Ndaki.

Mheshimiwa Naibu Waziri ameyasema hayo katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Babati katika Baraza la Kwanza la Madiwani wa Halmashauri hiyo lililofanyika jana tarehe 11 Novemba 2020.

“Ndugu zangu, nimshukuru sana Mhe. Rais, haikuwa kazi nyepesi kwani kati ya Wabunge zaidi ya Mia tatu nami kupatikana miongoni mwao, sio kazi nyepesi” alisema Mh. Gekul.

Sambamba na shukrani hizo, ameendelea kusema kuwa katika upande wa uvuvi Mkoa wa Manyara tayari wawekezaji kutoka china wamejitokeza katika Ziwa Manyara hivyo kazi inayoendelea ni pamoja na ufugaji wa samaki katika vizimba. Lakini amewataarifa wavuvi kukutana na hao wataalamu (wawekezaji) ili kujadili mambo mbalimbali yahusuyo uwekazaji huo.  

Uwekezaji huo katika Sekta ya uvuvi utapelekea upatikanaji wa ajira kwa wananchi na pia Halmashauri zitajinufaisha katika kujipatia mapato na pia kutapelekea upatikanaji wa Samaki wa kutosha katika mji wa Babati.

Hata hivyo, katika ajira zaidi ya milioni nane zilizoahidiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri Ya muungano wa Tanzania, Naibu Waziri huyo amesema sekta ya Uvuvi imetakiwa itengeneze ajira zaidi ya elfu arobaini na tano nchi nzima ili kuimarisha, kukuza na kuboresha sekta hiyo.

Maneno hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Paulina Gekul leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumalizika kwa baraza la Madiwani.

Naye Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg Halfan Matipula amemuasa Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Madiwani Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Maisaka Bw. Abrahman H. Kololi kuwa mshikamano na ushirikiano na madiwani wenzake pamoja na katibu wake ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Fortunatus Hilary Fwema ndiyo utakuwa chanzo kikubwa cha mafanikio katika Halmashauri.

“Ili tufanikiwe, Mhe Mwenyekiti ni muhimu sana kutambua kuwa hakuna mafanikio yoyote ambayo yanakuja bila mshikamano, ninayo Imani kubwa sana na wewe utashikamana na madiwani wako lakini pia utashikamana na katibu wako ambaye ni mkurugenzi wetu wa Halmashauri ya Mji”. Alisisitiza Katibu Tawala


Mheshimiwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi(kushoto) Bi. Pauline Gekul akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Babati Ndg. Halfani Matipula.


Pamoja na hayo, Baraza la Madiwani limefanya Mkutano wake wa kwanza wa Baraza uliohudhuriwa na wananchi kutoka sehemu mbalimbali za mji wa Babati katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya mji. Katika Baraza hilo, zoezi la kuapishwa Madiwani lilifanyika likiambatana na uchaguzi wa viongozi (Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na makamu wake) ambapo Mhe. Kololi kuibuka kidedea na kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kupata kura zote zilizopigwa na waheshimiwa madiwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bw. Abrahman Hussein Kololi.


Naye Mhe. Hiiti Qambalali Mutho Diwani wa Kata ya Bonga alitangazwa kuwa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo baada ya kuzoa kura zote zilizopigwa na waheshimiwa madiwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati (Kulia) Bw. Abrahman Hussein Kololi akiwa Makamu wake (kushoto) Bw. Hiiti Qambalali Mutho.


(Picha zote na Nyeneu, P. R ) 


Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR CONSTRUCTION SUPERVISION CONSUTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BABATI TOWN UNDER TACTIC PRJECT TIER 2 March 07, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili 2025. May 08, 2025
  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Mji Babati imefanya Ziara kukagua Miradi ya Maendeleo

    May 07, 2025
  • Watumishi Manyara wametakiwa kupendana na kuacha chuki.

    April 30, 2025
  • Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amewataka Wananchi kuuenzi Muungano.

    April 26, 2025
  • Chanjo nyongeza ya polio (IPV2) kuanza kutolewa kwa watoto wa miezi 9 mwezi wa tano 2025.

    April 24, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Babati 2024
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati