Baraza la Madiwani kwa robo ya nne ya mwaka 2023/2024 limefanyika katika Halmashauri ya Mji wa Babati ambalo limeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mhe. Abdulrahman H.Kololi na limehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti, Waheshimiwa Madiwani,Mkurugenzi,Wataalam na waalikwa wengine katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Katika Baraza hilo Madiwani kutoka Kata zote 8 zilizopo katika Halmashauri ya Mji wamewasilisha taarifa ya utekelezaji katika Kata zao kwa kipindi cha robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 na taarifa hizo zote zimepokelewa.
Mhe. Kololi amepongeza kuhusu ukusanyaji wa mapato kuwa umeendelea vizuri ametaka jitihada zaidi ili kuongeza mapato na hatimaye kupitia mapato miradi ya maendeleo kukamilka kwa wakati na kuendesha shughuli nyinginezo zilizopo katika Halmashauri kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mji wa Babati CPA Shaaban ameahidi kuongeza nguvu zaidi katika ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufika katika malengo makubwa kwa kutumia njia tofauti tofauti ikiwemo kuwafuatilia kwa ukaribu wakusanyaji wa mapato.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati