Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA Shaaban A. Mpendu amewaongoza Wananchi wa Mtaa wa Bagara Ziwani kupiga kura na kuwataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kuchagua Viongozi wanaowataka.
Pia amesisitiza kuwa Uchaguzi wa Serikali za mitaa ndio msingi wa Serikali kuu na ni kiunganishi baina ya Serikali na Wananchi hivyo amewataka wananchi wasiipoteze haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka. Ameongeza kuwa Vituo vimefunguliwa saa 2:00 Asubuhi na vitafungwa saa 10:00 jioni.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati