Mkuu wa Wilaya wa Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Manyara kujitokeza kuboresha taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kwenye vituo vilivyopo karibu na makazi yao ni fursa kikatiba na haki ya msingi kushiriki katika zoezi hilo ambalo limeendelea katika Jimbo la Uchaguzi Mkoani Manyara.
Pia amesema kuwa zoezi halichukui muda mrefu hivyo wananchi wanaweza kujitokeza na kujiandikisha kwa muda mfupi kisha kurejea katika majukumu ya kila siku na ametoa wito kwa wale wote ambao wamefikisha umri wa miaka 18 kuendelea kujitokeza kujiandikisha ili ifikapo Uchaguzi wa Mwaka 2025 kuchagua Viongozi wanaowahitaji kuliongoza Taifa.
Vilevile Mhe.Emmanuela amepata wasaa wa kuboresha taarifa katika moja ya kituo vilivyopo katika Jimbo la Babati Mjini.Amesisitiza kuwa wananchi wametakiwa kuendelea kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2025.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati