Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuella Kaganda amewataka Wananchi kupiga kura kwa amani na utulivu ifikapo tarehe 27 Novemba 2024, Mhe. Kaganda ameyasema hayo katika Bonanza la Uchaguzi la kuhamasisha watu kujitokeza kupiga kura. lililofanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa,
Katika hotuba yake Mhe.kaganda ameeleza kuwa "uchaguzi ni zoezi la kidemokrasia wananchi wote wenye sifa mkapige kura mchague Viongozi wanaofaa, watakaosaidia kuleta Maendeleo" pia ameongeza kuwa zoezi la kupiga kura litatumia masaa nane tu kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi jioni.
Wananchi wamejitokeza kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo kufukuza kuku, riadha, kukuna nazi, Mpira wa pete, Mpira wa miguu, Mpira wa kikapu,kula mikate na soda na Mbio za kwenye Magunia,.
Sambamba na hilo Mkuu wa TAKUKURU(Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa) Mkoa wa Manyara Bw. Bahati Haule amewataka Wananchi waepukane na Rushwa hasa kipindi hiki cha Uchaguzi, kwakuwa Rushwa ni adui mkubwa wa Maendeleo na haki.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati