Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuella Kaganda amewataka Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Babati kusimamia miradi ya maendeleo kwa ufanisi ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Babati.
Aidha Mhe. Kaganda amezungumzia mikopo ya Halmashauri ya 10% na kutoa wito kwa Idara ya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha mchakato wa utoaji mikopo umefanyika kwa uwazi na ushirikishi wa wananchi na amesisitiza kuwa ni muhimu kwa watu wote wenye sifa kupata mikopo hiyo bila kubaguliwa ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii.
Vilevile Mhe. Kaganda ameagiza maafisa ushirika kuhakikisha kila Kata inakuwa na Chama cha Ushirika wa Mazao (AMCOS) ifikapo Februari 2025 na amesisitiza kuwa AMCOS zitachangia katika kuongeza kipato kwa wakulima na kusaidia kuinua uchumi wa jamii kwa ujumla na ameongeza kuwa Maafisa ushirika kufanya kazi kwa ukaribu na Madiwani ili kutimiza lengo hilo kwa ufanisi.
Mhe.Kaganda amewataka Madiwani kuendelea kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika Tarehe 27/11/2024.
Sambamba na hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe. Abdulrahman Kololi amemshukuru Mkuu wa Wilaya na kuahidi kuwa Waheshimiwa Madiwani watatekeleza maagizo hayo.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati