Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amefanya ziara katika Kata ya Bonga Halmashauri ya Mji wa Babati ili kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzitatua kero hizo. Mhe.Sendiga amewaeleza Wananchi kuwa Serikali ya Tanzania ni sikivu na ipo kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili.
Katika mkutano huo kero kubwa iliyotajwa na Wananchi wa Mtaa wa Haraa wameeleza ni ukosefu wa umeme katika mtaa wao, jambo lililopelekea Mhe. Sendiga kutoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Tanesco kuhakikisha ifikapo tarehe 15 Disemba wananchi hao wawe wamefikiwa na umeme.
Aidha Diwani wa Kata ya Bonga Mhe.Hiiti Qambalali Mutho amewaelezea Wananchi maendeleo makubwa yaliyopatikana kwa kipindi cha Uongozi wa awamu ya Sita, akitaja mafanikio kama vile huduma za maji kwa kaya zote, Ujenzi wa Shule za Sekondari na Shule za Msingi, Ujenzi wa Vituo vya afya na Zahanati, pamoja na mikopo ya 10% ya Halmashauri inayowanufaisha Wananchi na ameeleza kuwa maendeleo haya yameleta mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi wa kata hiyo.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati