Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga ameongoza wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura katika Kituo cha Mtaa wa Mrara Kata ya Babati.
Mhe.Sendiga amewataka Wananchi wote wenye sifa ya kujiandikisha na kuhakikisha hawapotezi fursa hiyo ya kujiandikisha kwa kuwa inatumia muda mfupi na hakuzuii Wananchi kuendelea na shughuli za maendeleo zoezi limeanza rasmi tarehe 11/10/2024 hadi 20/10/2024.
Pia Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Babati CPA Shaaban A. Mpendu amejiandikisha katika Kituo cha Ofisi ya Mtaa wa Bagara Ziwani na ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika siku hizi za mwanzoni ili kuondoa msongamano wakati wa siku za mwishoni.
Aidha Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Babati ametoa ufafanuzi kuhusu zoezi lililopita na hili na amesema kuwa uandikishaji wa sasa ni maalum kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uandikishaji uliofanyika mwezi Septemba ni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu.
Sambamba na hilo amewataka Wananchi wenyesifa kujitokeza kujiandikisha mapema wasisubiri tarehe za mwishoni.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati