Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura umeudhuriwa na Mhe.Jaji Asina A.Omari,Mwakilishi wa Mkurugenzi Bi.Giveness Aswile,Mhe.Balozi Omary R.Mapuri,Viongozi wa Vyama vya Siasa,Asasi za Kirai,Taasisi za Serikali na wadau mbalimbali katika Ukumbi wa Mkutano Ofisi ya MKuu wa Mkoa wa Manyara.
Katika Mkutano huo mada zimetolewa ili kutoa elimu juu ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na mfumo wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na vifaa vinavyotumika katika zoezi hilo.Ambapo wadau watakuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa wananchi na kuwahamasisha kujitokeza kujiandikisha katika zoezi hilo.
Mhe.Jaji Asina Omari ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha na kuboresha taarifa ifikapo tarehe 4/09/2024-10/09/2024 katika vituo vitakavyokuwepo kwenye makazi yao kwa wale wote wenye vigezo vya kuwa mpiga kura ‘’Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora''.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati