Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi.Pendo Mangali amefungua mafunzo ya njia bora ya uagizaji,utunzaji na ujazaji wa nyenzo za utunzaji kumbukumbu za bidhaa za Afya kwa Waganga Wafawidhi wa Halmashauri ya Mji wa Babati,Mafamasia wa Hospitali ya Mji, Vituo vya afya na Zahanati katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Katika Mafunzo hayo mada mbalimbali zimetolewa ili washiriki waweze kuelewa na kufanyia kazi makubaliano ambayo yamefikiwa baada ya mafunzo ambapo mada ya Nyenzo za utunzaji wa kumbukumbu za bidhaa za afya, Miongozo mbalimbali ya Serikali kama vile[mwongozo wa matibabu,orodha ya bidhaa muhimu za afya,mwongozo wa kamati za tiba na dawa,mwongozo wa mshitiri na mwongozo wa matumizi ya fedha za bidha za afya],Mifumo ya uagizaji wa bidhaa za afya na uchakataji wa taarifa za matumizi ya bidhaa za afya na kufanya maamuzi kwa kutumia takwimu.
Vilevile Bi.Pendo Mangali amesisitiza juu ya ukaguzi wa manunuzi yanayofanyika katika Vituo vya kutolea huduma za Afya katika ngazi zote wakati wa ujio ya vifaa tiba na vitendea kazi vingine. Pia amewapongeza kwa kazi nzuri na amewataka kuboresha zaidi huduma zinazotolewa katika Vituo vya kutolea huduma za Afya wananchi wanawategemea sana.
Aidha washiriki wametakiwa kuwa makini katika kujifunza ili kuweza kuwasaidia katika utendaji wa majukumu ya kila siku katika vituo vya kazi na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi wakati wote.
Pia Mganga Mfawidhi wa Bonga Dk.Dalabe kwa niaba ya Washiriki wote amemshukuru sana Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji Bi. Pendo Mangali kwa kujumuika nao pamoja katika mafunzo na amesisistiza kuwa ushauri wameupokea na wataufanyia kazi ili kuendelea kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi wakati wote katika Vituo vya kazi.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati