Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA Shaaban A. Mpendu amewapongeza wananchi wa Jimbo la Babati Mjini kwa kuendelea kujitokeza Kujiandikisha na Kuboresha taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika Vituo vilivyopo kwenye makazi yao Mkoani Manyara.
Pia CPA Mpendu ametoa wito kwa wananchi ambao bado hawajajiandikisha kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa katika Daftari la Wapiga Kura ili waweze kupata nafasi ya kumchagua kiongozi wanaemtaka katika Uchaguzi wa Mwaka 2025 ni haki ya Msingi.
Aidha CPA Shaaban ameboresha taarifa zake katika moja ya Kituo kilichopo Jimbo la Babati Mjini na kupatiwa kadi ambayo inampa nafasi ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 katika JImbo la Babati Mjini.
Vilevile Mawakala waliopo katika Vituo vya Kujiandikisha wamesema kuwa mwitikio ni mkubwa na wamewahimiza Vijana kuendelea kujitokeza kwa wingi zaidi katika Kujiandikisha na kuboresha taarifa katika Daftrai la Kudumu la Wapiga Kura.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati