Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange ameongoza zoezi la usafi katika Kijiji cha Singu Kata ya Sigino Halmashauri ya Mji wa Babati barabara ya kuelekea Singida, Viongozi mbalimbali ,wataalam na wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Babati wameshiriki katika zoezi la ufanyaji usafi Mkoani Manyara.
Pia katika zoezi hilo Mhe.Twange amesisitiza juu ya ufanyaji wa usafi katika maeneo yetu tusisubiri tu hadi viongozi inapendeza mazingira yetu yakiwa safi. Na amesisitiza pia juu ya upandaji miti katika maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya kupanda miti.Na amesema kuwa kuna sheria ndogo ya usafi itaanzishwa hivyo Viongozi wa ngazi ya chini wawe tayari kushirikiana ili sheria hiyo iweze kufanya kazi na Halmashauri ya Mji kuzidi kuwa safi zaidi.
Vilevile amempongeza Mwenyekiti wa Kijiji cha Singu na wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la usafi huo ni uzalendo kufanya usafi kwa umoja na kushirikiana na amesema kuwa watashughulika na wamiliki wa mabasi ili kuona namna watakavyowathibiti wasitupe taka barabarani.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi. Pendo Mangali amewapongeza wananchi na wataalam kushiriki katika zoezi hilo na amesema zoezi hilo ni kata kwa kata hadi kuhakikisha Halmashauri ya Mji inakuwa safi muda wote
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati