Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga ameambatana na timu yake ya Wataalam pamoja na Viongozi katika kutatua mgogoro wa ardhi Dudumera ambapo mgogoro huo umedumu takribani miaka 5 ukihusisha Vijiji vya Malangi na Kiru vilivyopo Wilayani Babati dhidi ya Mwekezaji Mkoani Manyara.
Mhe.Sendiga amewapatanisha pande zote mbili na amewataka wananchi hao kuacha tabia ya uvamizi katika maeneo ambayo si ya kwao ni ya Mwekezaji,pia amewahimiza kuacha kulima katika maeneo hayo na kusubiri kupewa maeneo mengine ili waendelee na shughuli zao za kilimo pasipo kuwa na mgogoro.
Ameongeza kuwa kwa yeyote atakayevunja amani atashughulikiwa mara moja na amesisitiza wametakiwa kuishi kwa amani na upendo na ndio nguzo kubwa ya maendeleo katika Kijiji.Vilevile amemuhakikishia Mwekezaji pamoja na jamii kwa ujumla usalama upo.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema kuwa wananchi wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza mazingira na kuacha kufanya uharibifu kwa kukata miti na kuchoma mkaa kwa kufanya hivyo kunasababisha mazingira kuwa mabaya.
Sambamba na hilo Mhe.Sendiga ameahidi kushughulikia changamoto za Maji,Umeme pamoja na Shule katika Kijiji hicho na Ujenzi wa Shule utakapoanza ameahidi kuchangia mifuko 30 ya saruji na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe.Kololi ameahidi kutoa mifuko 20 ya saruji.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati