Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amekabidhi vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Mkoa na Halmashauri ya Mji wa Babati ambavyo vitarahisisha utendaji kazi kwa Maafisa ugani zoezi hilo limefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Mhe Sendiga amekabidhi gari,vishikwambi na mavazi(uniform)vitakavyosaidia utendaji wa kazi,ameongeza kuwa gari litasaidia usimamizi wa mazao katika Mkoa wa Manyara na ametoa shukrani za dhati kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa vitendea kazi hivyo.
Pia ametoa wito kwa wakulima kuendelea kupeleka mazao katika maghala ili mazao hayo yauzwe kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa bei nzuri na isiyo na maumivu kwao na kupata faida ya kujishughulisha na kilimo na amewataka madalali kufika kwenye minada ili kununua mazao.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati