Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amezungumza na waandishi wa Habari katika kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2024 ametoa maelekezo kuwa kwa Wilaya zote katika Mkoa wa Manyara kufanya matembezi /jogging mkutano huo umefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Mhe.Sendiga amesema kuwa matembezi/jogging imepewa jina la Manyara Daftari Dei chini ya kauli mbiu Imarisha Afya yako jiandikishe na kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Jamii endelevu siku ya tarehe 1/09/2024 dhumuni ni kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari na kuboresha taarifa ifikapo tarehe 4/09/2024 kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kushiriki katika Uchaguzi.
Mhe.Queen ameongeza kuwa washiriki katika matembezi/jogging ni Wananchi,Watumishi wa Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali na matembezi yataanzia katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa,kuzunguka eneo la Mji wa Babati na kuhitimishwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa ambapo viburudisho mbalimbali vitakuwepo kwa washiriki wote. Na ametoa wito kwa Wananchi na Taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tukio hilo.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati