Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amefungua maadhimisho ya Siku ya mbolea Duniani yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Manyara,maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Stendi ya zamani kauli mbiu “Tuongee Mbolea,Kilimo ni Mbolea”.Katika ufunguzi ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Bunge Viwanda,Biashara na Kilimo pamoja na Viongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa,Wilaya na Halmashauri.
Aidha katika maadhimisho hayo Mhe.Sendiga ameishukuru Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) kwa kufanya maadhimisho hayo Mkoani Manyara ameongeza kuwa Manyara ni sehemu sahihi kwa kuwa ni Mkoa wenye rutuba inayoweza kuzalisha mazao mbalimbali kama vitunguu maji,dengu,vitunguu swaumu,alizeti,miwa pamba,shayiri,mahindi,mpunga na ngano.
Pia amewataka Mawakala wa Mbolea kusogeza huduma maeneo ya vijijini kwa wakulima ili kuwapunguzia gharama za usafirishaji wa mbolea na ametoa wito kwa Wananchi kutembelea mabanda ya mbolea ili wapate elimu ya namna sahihi ya matumizi ya mbolea pamoja na mbegu.
Sambamba na hilo amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mbolea za ruzuku na mbegu za ruzuku ili kumsaidia mkulima kuweza kulima kilimo chenye tija.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati