Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga, Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Mkurugenzi Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA),Viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Manyara, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Watumishi wamehudhuria hafla ya uwekaji saini katika mikataba 6 ya Ujenzi miradi ya maji yenye thamani ya Billioni 9 ambapo hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara.
Mhe. Sendiga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya jitihada kubwa za kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji Mkoani Manyara, kwa kupeleka Ujenzi miradi ya maji kwa wananchi.
Aidha amesisitiza wakandarasi kukamilisha Ujenzi wa miradi hiyo kwa wakati na amewataka Wakuu wa Wilaya kusimamia Ujenzi miradi na kuangalia mikataba ili kumaliza miradi kwa wakati.Pia ameongeza kuwa Mkoa wa Manyara una wastani wa asilimia 70.5 kwa upatikanaji wa maji na Mkoa wa Manyara una Ujenzi miradi mikubwa ya maji takribani 28.
Vilevile amesema kuwa Ujenzi wa miradi ya maji imeinua Sekta ya ufugaji katika Mkoa ikiwemo Ujenzi wa josho za kuoshea mifugo katika Wilaya kwa kipindi cha miaka 3 ya Uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Mkoa umepokea jumla ya Bilioni 56 kwa ajili ya utekelezaji wa Ujenzi wa miradi ya maji. Aidha kwa bajeti ya mwaka 2022 -2023 Mkoa umepokea jumla ya Bilioni 21.7 kwa ajili Ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa.
Sambamba na hilo amesisitiza kuwa Taasisi za Serikali kulipa bili za maji kwa wakati huku akiwataka wakandarasi kuajiri wazawa katika miradi hiyo na ikalete maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi ikiwemo wajasiriamali wadogo kama mama lishe.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati