Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amemuapisha Bw.Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara.Aidha Bw.Fakii hapo awali alikuwa ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi [UVCCM].Uapisho huo umefanyika katika Ukumbi wa mikutano Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Bw.Fakii amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi huo amepokea kwa furaha sana na hekima kubwa ameahidi kutekeleza yale yote atakayoagizwa pamoja na majukumu mengine.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Sendiga amewahimiza Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Manyara pamoja na Viongozi wengine kuhakikisha miradi ya kimkakati na ya maendeleo inatekeleza na kukamilika kwa wakati.Pia ameongeza kuzingatia suala la ukusanyaji wa mapato na mgawanyo wa 40% ya mapato ya ndani.
Mhe. Sendiga amesisitiza kusikiliza na kutatua kero za Wananchi hasa migogoro ya ardhi.Vilevile amewataka Viongozi kudumisha mahusiano baina ya Taasisi binafsi na za Umma katika kuleta maendeleo.
Pia ameongeza kuwa utoaji wa taarifa kwa wananchi juu ya mapato, matumizi na shughuli za Serikali katika Kijiji kwa kufanya mikutano ya hadhara pamoja na vikao na Wananchi.Ili waweze kujua na kutambua miradi yote ya maendeleo iliyopo katika Kijiji ,Kata au Mitaa.
Sambamba na hilo Mhe.Sendiga ametaka fedha zote za makusanyo ziwekwe benki,kuhakikisha Wananchi wanapata Huduma bora katika sekta ya Maji,Shule pamoja na Afya,Kuweka mikakati katika kukomesha na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi na kugombea nafasi za Uongozi hasa Wanawake.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati