Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Manyara wamefanya mkutano na waandishi wa habari pamoja na Wataalam kutoka Taasisi tofauti ambapo lengo kuu ni kuutarifu Umma juu ya mafanikio ambayo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameyaleta kwa wananchi wa Mkoa wa Manyara mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Kisora Royal Hall Mkoani Manyara.
Mhe.Sendiga amesema kuwa Mkoa wa Manyara una idadi ya watu takribani Millioni 1.8 .Na ameongeza kuwa Mkoa umepokea kiasi cha shillingi Billioni 559 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika Sekta Afya,Elimu,Maji,Umeme,Miundombinu ya Barabara ,Ujenzi wa Soko la madini Mererani pamoja na stendi ya mabasi Wilaya ya Hanang’.
Pia Mhe.Mkuu wa Mkoa amepata wasaa wa kujibu maswali kadhaa kutoka kwa waandishi wa habari wa vyombo tofauti lengo ni kwaaelezea namna Serikali ya awamu ya Sita inavyotekeleza majukumu yake katika ngazi za chini mpka juu.Amewataka waandishi kutumia kalamu zao pia kutao elimu kwa wananchi kuhusu masuala kadhaa ya usalama kama vile kwa wale wananchi wanaoishi karibu na hifadhi kumetokea ongezeko la wanyama hivyo wametakiwa kuchukua tahadhali zaidi katika maeneo hayo.
Aidha amesisitiza kuwa wananchi ambao wamekuwa na tabia ya kuibua migogoro upya kila anapokuja kiongozi mpya kuacha tabia hiyo mara moja kwa sasa wataanza kushughulika na wao kabla ya kushughulikia hiyo changamoto maana migogoro inakuwa haifiki mwisho.Vilevile suala la umeme taarifa itaendelea kutolewa na mamlaka husika juu ya changamoto hiyo na ameongeza kuwa suala la ukatili wa kijinsia na Ukeketaji linaendelea kupungua.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati