Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amefanya kikao na madereva wa bodaboda, bajaji, machinga na mama Lishe katika Ukumbi wa Whiterose Babati. Kikao hicho kimeudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Mhe. Karolina Mthapula, Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe Lazaro Twange, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Pendo Mangali pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Mhe. Queen Sendiga amefanya kikao hicho ili kuwafahamisha juu ya maandalizi ya sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,Kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere pamoja na maonesha ya wiki ya vijana Kitaifa. Ambapo amewahimiza juu ya hutoaji wa huduma bora kwa wageni wanaotarajiwa kuhudhuria katika matukio hayo ya Kitaifa.
Aidha Mhe. Sendiga amewasisitiza kutumia fursa hiyo adimu kwa kuboresha mazingira ya hutoaji huduma zao ikiwa ni madereva bodaboda kuwa wasafi, kuendesha vyombo vya moto kwa uangalifu na mama lishe kuzingatia usafi wakati wa kuandaa chakula.
Pia katika kikao hicho ametoa kiakisi mwanga { reflactor} kwa ajili ya madereva wa bodaboda na bajaji kwa usalama wao pindi wanapokuwa barabarani,vilevile amewataka madereva wa bodaboda kuwa na ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa pindi wanapoona dalili za watu wasio waadalifu wakati wa matukio hayo kwani kutakuwa na mwingiliano wa watu wengi.
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amewaruhusu madereva wa bodaboda,bajaji,machinga pamoja na mama lishe kuingia ndani ya uwanja wa Kwaraa ili kujionea jinsi ya shughuli za Ujenzi wa Uwanja huo unavyoendelea na kuwaomba kuutunza pindi utakapokamilika.Ameongeza kuwa uwanja huo ni mali ya wananchi wa Mkoa wa Manyara.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati