Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amewakaribisha rasmi Wanafunzi katika Shule Mpya ya Wasichana ya Mkoa wa Manyara iliyopo katika Kijiji cha Kiongozi Kata ya Maisaka Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo mpaka sasa wanafunzi takribani 118 wamewasili na kuanza masomo ya Kidato cha Tano katika mchepuo wa Sayansi (PCM na PCB).
Mhe. Sendiga amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kutimiza malengo katika maisha na amewahakikishia usalama wa kutosha wakati wote wanapokuwa mazingira ya Shule hivyo wanatakiwa kuwa na nidhamu na heshima kwa walimu na walezi.
Pia Mhe.Queen amewashukuru na ametoa pongezi kwa wazazi na walezi waliopeleka wanafunzi katika Shule hiyo mpya ya Wasichana Mkoa wa Manyara na amewahakikishia wanafunzi hao wapo sehemu sahihi na watapata Elimu bora.
Aidha Mhe.Sendiga ameagiza umaliziaji wa miundombinu ambayo haijakamilika hasa bwalo ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao pasipo na changamoto wanapokuwa katika mazingira ya Shule.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati