Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Damas Daniel Ndumbaro ametembelea katika eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Michezo katika umahiri wa Riadha Kanda ya kaskazini Mkoani Manyara.
Katika ziara hiyo ameambatana na timu kutoka katika Baraza la Michezo Tanzania,Mhe Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul,Kaimu Katibu Tawala Bw.Dominic Mbwette,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe.Abdurahman H.Kololi,Kaimu Mkurugenzi Bw.Simon Mumbee pamoja na Viongozi mbalimbali.
Mhe.Ndumbaro amesema kuwa katika Kituo hicho cha michezo kutakuwa na viwanja vya michezo yote mpira wa miguu,mpira wa pete na mpira wa mikono.Na ameongeza kuwa Vituo hivyo vitajengwa katika Kanda zote ili kuweza kuwapa wachezaji ,muda zaidi ya kujiandaa katika mashindano ya michezo kwa kukaa katika makambi ambapo katika Vituo hivyo kutakuwa na hosteli.
Aidha amesema kuwa kwa sasa Michezo ni ajira na uchumi hivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.Samia Suluhu Hassan ameliona hilo na ametoa maagizo juu ya utekelezaji wa ujenzi wa Vituo vya Michezo kwa Kanda zote na ujenzi wa Kituo hicho kwa Kanda ya Kaskazini utaanzaa katika mwaka huu wa fedha.Vilevile Mhe.Ndumbalo amekagua mipaka ya uwanja na ameridhishwa na eneo la ujenzi wa Kituo hicho.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha amesema,ujenzi huo utaanza kutekelezwa katika Mwaka huu wa fedha 2024/2025 ambapo tayari fedha imeshatengwa na mchakato wa kumpata mshauri elekezi umefikia hatua za mwisho.
Sambamba na hilo Mhe.Ndumbalo na Timu yote wametembelea Uwanja wa Tanzanite Kwaraa amepongeza kwa ujenzi mzuri na wa kisasa wa uwanja huo ametaka kuufanyia marekebisho ili Timu kubwa ziendelee kutumia uwanja katika mechi kubwa.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati