Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe. Abdulrahman H. Kololi ameliongoza Baraza la Madiwani la kawaida katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo Baraza hilo limeudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi.Pendo Mangali,Madiwani wa Kata zote,Wataalam,Viongozi wa Taasisi,Katibu wa Chama cha Mapinduzi Halmashauri ya Mji pamoja na waalikwa wengine.
Mhe.Kololi amesisitiza sana juu ya suala la lishe katika Shule,ili Wanafunzi wasome kwa bidii na kufanya vizuri lazima lishe iwepo ya kutosha amewataka Madiwani wote kuwakumbusha Wazazi kutoa chakula kwa wakati ili kusilete changamoto yoyote kwa Wanafunzi wanapokuwa Shule.
Pia Mhe.Kololi ametoa pongezi katika usafi wa mazingira kwa kuwapongeza Idara husika juu ya zoezi la kuweka Mji katika hali ya Usafi imesaidia kuepukana na magonjwa na ameongeza kuwa Mji unapendeza unapokuwa msafi na ni wajibu wetu sote kuweka Mji safi.
Aidha Mhe.Abdulrahman ameongeza kuwa Halmashauri imejitahidi katika kukusanya mapato ambayo yatasaidia katika shughuli za maendeleo ya Halmashauri ya Mji amewapongeza wataalam na amewataka kuendelea na ukusanyaji huo wa mapato.
Vilevile kila Diwani amewasilisha taarifa ya utekelezaji katika Kata zao pamoja na kubainisha changamoto zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa na kupata majibu. Takribani taarifa ya Kata zote 8 zilizopo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Babati Madiwani wamewasilisha taarifa katika Baraza hilo la kawaida la Madiwani.
Pia Ndugu Mohamed Cholange Katibu wa CCM Halmashauri ya Mji amewapongeza Timu ya Wataalam kwa kazi nzuri katika kila Idara na Vitengo amewataka kutokuchanganya Siasa na Utaalam wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa weledi.
Sambamba na hilo Mhe.Kololi amepongeza pia zoezi la usafishaji wa Ziwa Babati na kusema kuwa Ziwa limeonekana vizuri sasa na jitihada zimeendelea zaidi ili kuleta muonekano mzuri wa Ziwa.Na ameongeza kuwa kila Diwani akatimize wajibu wake katika Kata.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati