Halmashauri ya Mji wa Babati limefanya Baraza la Madiwani robo ya tatu katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe.Abdulrahman H. Kololi.Pia Baraza hilo limehudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati,Katibu Tawala Wilaya,Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi [CCM],Waheshimiwa Madiwani,Watendaji pamoja na Wataalamu.
Mhe. Kololi amewapongeza Watendaji na Wataalamu kwa ujumla kwa juhudi zao za kuweka Mji katika hali ya Usafi hadi kufanikiwa kushika nafasi ya pili katika mashindano ya usafi na utunzaji wa mazingira katika Halmashauri ya Mji wa Babati.Mhe. Kololi amesisitiza kuweka mkazo katika sheria ndogondogo ili Halmashauri kuendelea kuwa safi muda wote.
KatibuTawala Wilaya ya Babati Bw.Halfan Mtapula amesema kuwa kila Diwani katika Kata yake kuhakikisha anatoa taarifa ya upatikanaji wa chakula kwa kila Shule katika Kata.Vilevile amesisitiza fedha za mkopo wa asilimia 10 kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wamefanya marejesho ili kuwezesha vikundi vingine kupata mkopo.Na ameongeza kuwa usimamizi wa miradi uongezeke ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati.
Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi [CCM] Wilaya ya Babati Bi. Elizabeth Malley amepongeza suala la ukusanyaji wa mapato upo vizuri na katika usimamizi wa miradi yote ya maendeleo ipo katika viwango vizuri sana.Vilevile amesisitiza iendelee kusimamiwa kwa ukaribu ili ikamilike kwa wakati na amewataka Viongozi kuhakikisha miradi viporo pia inakamilishwa.
Pia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi.Pendo Mangali amesema kuwa Halmashauri ya Mji wa Babati imepata hati safi katika matumizi ya fedha mwaka 2023/2024.Vilevile ameongeza kuwa matokeo ya darasa la saba na kidato cha nne Halmashauri ya Mji imepata vyeti vya pongezi kwa ufaulu mzuri zaidi wa wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari 2023.Pia amesisitiza kuanza kwa maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi wa 10.
Sambamba na hilo Mhe. Kololi amesisitiza kila kiongozi kutimiza majukumu yake ya kazi na amewataka Madiwani kuhakikisha kila Shule katika Kata Wanafunzi wamepata chakula.Pia ameongeza kuwa Shule za Sekondari kwa kidato cha 5 na 6 ziongezeke ili wanafunzi wasipate changamoto ya kutembea umbali mrefu.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati