Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe. Abdulrahman Kololi amewataka Watendaji na Wasimamizi wa miradi ya maendeleo kusimamia kwa umakini miradi ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwanufaisha Wananchi amesema hayo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati katika Baraza la Madiwani ambalo limeudhuriwa na Makamu Mwenyekiti,Madiwani,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati,Wataalam pamoja na Watendaji wa Kata.
Mhe. Kololi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa pesa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na ameeleza kuwa katika kipindi cha Uongozi wa Awamu ya Sita Serikali imetoa pesa nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Mji wa Babati kama vile Ujenzi wa Hospitali ya Mji na ukarabati wa baadhi ya majengo, Ujenzi wa Zahanati, Shule za Sekondari, Shule za Msingi na uboreshaji wa miundombinu ya maji.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Babati CPA. Shaaban Mpendu ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu Serikali imetoa fedha za miradi ya maendeleo katika Sekta ya Elimu,Afya,Maji na miundombinu ya Barabara takribani Bilioni 24.
Sambamba na hilo Madiwani wa Kata zote 8 wamewasilisha taarifa za utekelezaji katika Kata zao kwa robo ya kwanza katika Baraza la Madiwani.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati