Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuella Kaganda amefanya kikao na Kamati ya Lishe ya Wilaya ambapo kimeudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA Shaaban Mpendu,Maafisa Lishe pamoja na Watendaji wa Kata katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Mhe.Emmanuella Kaganda amewataka Watendaji wa Kata na Maafisa lishe kusimamia kwa umakini uwepo wa lishe bora kwa watoto na upandaji wa miti ya matunda pamoja na bustani za mboga katika mazingira ya shule.
Aidha Mhe.Kaganda ametoa wito na amesisitiza umuhimu wa kuimarisha lishe bora shuleni kama njia ya kuongeza afya na uwezo wa kujifunza kwa wanafunzi.Na ameongeza kuwa kuwepo wa bustani za mboga na miti ya matunda shuleni kutawezesha watoto kupata lishe yenye virutubisho vya kutosha kwa kuimalisha afya zao na kuendeleza jamii yenye afya bora.
Pia Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Laurensia Urio, amebainisha kuwa hali ya lishe kwa sasa ni nzuri na ameeleza kuwa mkataba wa lishe unalenga kuhakikisha kuwa lishe bora imezingatiwa na kufuatiliwa kwa ukaribu katika maeneo yote ya Wilaya ya Babati.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati