Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuella Kaganda amehitimisha rasmi maonesho ya Biashara ya ‘Tanzanite Manyara Trade Fair’ yaliyofanyika kwa muda wa siku kumi katika Uwanja wa Stendi ya zamani Mjini Babati.
Mhe. Kaganda amesema kuwa maonesho hayo yamevutia idadi kubwa ya washiriki kutoka 232 mwaka jana hadi 422 kwa mwaka huu ambapo ongezeko hilo limeakisi maendeleo ya biashara na uchumi katika Mkoa wa Manyara.
Aidha amepongeza Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa mafanikio na ubunifu walionesha hadi kuwa washindi katika maonesho hayo na kupata vyeti vya pongezi.
Mhe.Kaganda amewapongeza wajasiriamali na Mamlaka mbalimbali zilizoshiriki katika maonesho kwa kuleta bidhaa na kutoa huduma zenye ubunifu wa hali ya juu.
Aidha Katibu wa Taasisi ya TCCIA Bi.Zainabu Rajabu amesema kuwa uwepo wa maonesho hayo umesaidia kuimarisha mzunguko wa fedha kufika zaidi ya shilingi Milioni 450 ndani ya kipindi cha maonesho na ameomba ushirikiano wa wadau wa Serikali na sekta binafsi katika maandalizi ya maonesho hayo kwa kuwa ni muhimu kwa maendeleo ya Biashara.
Sambamba na hayo Mhe. Kaganda ametoa wito kwa Halmashauri zote kushiriki kikamilifu katika maonesho ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa ndani na kuzihimiza Taasisi za kifedha kushirikiana na wajasiriamali na amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba 2024 amesema ni fursa ya kuchagua Viongozi wenye uwezo wa kusimamia Maendeleo katika ngazi ya jamii.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati