Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amefanya ziara ya kutembelea Kata ya Bonga Halmashauri ya Mji wa Babati kusikiliza kero za wananchi katika ziara hiyo ameambatana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Babati Mhe.Abdulrahman H.Kololi,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Simon Mumbee mkutano huo umefanyika katika Stendi ndogo ya Bonga.
Katika ziara hiyo amewataka Watendaji kuwa tambua watu wanaojitolea kataka Jamii ili kuleta chachu zaidi ya mabadiliko katika jamii na maendeleo ya Kata kukuwa na kuleta pia ushirikiano baina ya wanaojitolea pamoja na Watendaji wa Serikali kwa ujumla.
Pia ameongeza kuwa katika kusikiliza kero za wananchi ameambatana na Wakuu wa Taasisi na Wataalam ili kurahisisha utatuzi wa kero hizo na ni jambo jema kutatua kero ili jamii yetu ishi kwa Amani na kuendelea na majukumu ya kila siku pasipo na changamoto yoyote.
Vilevile ameaahidi kushughulikia migogoro ya ardhi kwa mtu yeyote atakayebainika ni chanzo cha huo mgogoro hata kama akiwa ni mtumishi wa Serikali au Wanakijiji kwa namna moja ama nyingne.Na amewasisitiza Watendaji kutenga muda wa kuwasikiliza Wazee ili kujua changamoto wanazopitia ili kuzitatu na sio kusubiri Mikutano ya hadhara.
Aidha Mhe.Sendiga ametoa zawadi ya gitaa lenye thamani ya Shilingi 400,000/=kwa mwimbaji wa mziki kutoka katika Kata ya Bonga.Pia amewataka Watendaji kutoa Elimu kuhusu TASAF ili wananchi kupata uelewa wa juu ya mnufaika kwa kushirikiana na wadau wanaoshughulikia TASAF.
Pia Mhe.Pauline Gekul amesema kuwa utafanyika uboreshaji wa Kituo cha Polisi Bonga,uchongaji wa Barabara na Ujenzi wa Soko utaanza ili kuboresha lililokuwepo na kurahisisha biashara kufanyika katika mazingira safi na salama. Na ameaahidi kushughulikia mgao wa Umeme katika Kata hiyo.
Sambamba na hilo ametembelea Ujenzi wa Ofisi ya Machinga, Ukumbi pamoja na matundu 3 ya vyoo ambapo amemtaka Kiongozi wa Machinga ifako tarehe 29/12/2023 kukabidhi Jengo na mnamo tarehe 29/01/2024 Jengo lizinduliwe na kutumika kwa wafanyabiashara
.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati