Baraza la Madiwani likiongozwa na Mhe.Abdulrahman H. Kololi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati limekutana leo katika ukumbi wa Mji wa Babati kujadili mihutasari ya kamati mbalimbali ya robo ya nne ya mwaka 2022/2023.
Mhe. Kololi amesisitiza sana kuhusu lishe,usafi wa mazingira na sehemu za kunywa maji shuleni ni muhimu kuwepo kwa kila shule za msingi na sekondari ili kulinda afya za wanafunzi ,walimu na watumishi wengine.
Aidha Mhe. Rose Muryang Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Singe ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuwezesha upatikanaji wa mawasiliano katika baadhi ya maeneo kwenye kata hiyo kwani mawasiliano yana umuhimu. Vilevile Baraza limempongeza Mtaalamu wa Mazingira kuwa usafi ndani ya Halmashauri yetu unazingatiwa na taka zinakusanywa kwa wakati na mwitikio wa wananchi ni mzuri na hakuna taka mitaani.
Vilevile Baraza limetaka kufahamu idadi kamili ya wanufaika wa TASAF ili kusaidia kujua Halmashauri ina watu wangapi wanawake kwa wanaume wanaonufaika pamoja na changamoto wanazopata wakati wakipatiwa huduma hiyo katika maeneo mbalimbali.
Pia Baraza hilo limejadili kuhusu kutengeneza vizimba kwa ajili ya samaki wanaokuwa wametoka kuvuliwa ili kuhakikisha afya kwa watumiaji wa samaki hao na utaratibu wa kukusanya ushuru kwa wavuvi uendelee.
Mhe. Kololi Mwenyekiti wa Halmashauri Mji wa Babati amewapongeza wataalamu wa afya, watendaji wa kata, wataalamu wa maendeleo ya jami, na waratibu wa elimu kata kwa kazi nzuri wanazofanya na kuwasisitiza kuendelea na majukumu hayo kwa weledi zaidi.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati