Mhe. Joyce Ndalichako Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar Bi,.Fatuma Hamad Rajab wamefanya ziara ya kutembelea Uwanja wa Kwaraa ambao kilele cha maadhimisho ya Mwenge wa Uhuru 2023 utafanyika Kitaifa.
Pia Mhe. Joyce Ndalichako ametoa pongezi kwa Viongozi wote wa Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana kwa hatua ya ujenzi huo ulipofikia amesisitiza usimamizi wa karibu ili kufika tarehe 30/09/2023 uwe umekamilika tayari kwa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.
Sambamba na ukaguzi huo ametoa wito kwa vijana kuonyesha vipaji vyao pamoja na kuwataka wananchi wa mikoa jirani kujitokeza kwa wingi siku ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 14 Oktoba 2023.
Vilevile Mhe. Joyce Ndalichako ametembelea Shule ya Sekondari Babati Day ambapo wanafunzi wa halaiki wanafanya mazoezi ya kuonyesha maumbo mbalimbali siku ya kilele cha Mwenge wa Uhuru.Pia amewapongeza walimu kwa mafunzo hayo na wazazi kwa kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika halaiki.
Katika ziara hiyo amekagua uwanja ambao utatumika katika wiki ya vijana pamoja na Kanisa Katoliki la Roho Mtakatifu ambapo ibada ya Misa Takatifu itafanyika katika siku ya kumbukizi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati